Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa na Uhusiano ya Kimataifa Ngemela Lubinga akimnadi Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM, jimbo la Buhigwe Felix Kavejuru, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Janda jimboni humo.


Buhigwe, Kigoma

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeahidi kwamba kitahakikisha mradi wa kuunganisha umeme katika vijiji vyote vya Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma unakamilishwa na Serikali kama ilivyooagwa.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa na Uhusiano ya Kimataifa Ngemela Lubinga amesema hayo kwa nyakati tofauti akiwa katika mikutano ya hadhara katika Kata ya Janda na Bukuba wakati akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Buhigwe, Felix Kavejuru.

Lubinga amesema tayari Vijiji 38 vimeunganishwa na umeme na bado vijiji 6 tu na hivyo CCM itahakikisha kupitia Serikali yake mradi wa kuunganisha umeme katika Vijiji vilivyobaki ikijumuisha Vijiji vya Janda na Mnyegera unakamilika haraka.

"Wananchi wa Buhigwe mnabahati sana kuwa na Mwalimu Kavejuru kama Mgombea wa Ubunge hapa, naomba mmpe kura zote za ndio, ili maendeleo yaje hapa Buhigwe kwa kasi", amesisitiza Lubinga

Akiwaomba kura wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo la Buhigwe kwa tiketi ya CCM Felix Kavejuru, ameendelea kuahidi kuwa atakuwa mnyenyekevu, mfuatiliaji na mtumishi mwema kwa wananchi wa Buhigwe.

Mikutano ya Kampeni ya CCM katika Jimbo la Buhigwe Mkoani Kigoma imeendelea, kwa ajili ya Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi iliyoachwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Dk. Philip Isdori Mpango kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...