wananchi watakiwa kuwaombea viongozi wa serikali pamoja naTaifa hususani katika kipindi hiki Cha mfungo wa Ramadhani ili amani iliyopo nchini iendelee kudumu .
wakizungumza viongozi wa dini wilayani Gairo mkoani Morogoro katika Dua ya kuliomba Taifa pamoja viongozi wa serikali wamesema viongozi wanatakiwa kuombewa ili waweze kuongoza Taifa katika misingi yenye Amani na Upendo ushirikino na kuwa na hofu ya Mungu .
Aidha kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Gairo Sirieli Nchembe amesema amani iliyopo nchini ni kutokana na viongozi waliopo madarakani pamoja na wananchi wanayo hofu ya Mungu huku akawaomba wananchi hao kushirikiana katika shughuli zote za kulijenga Taifa na kuwaombea wenye uwezo wa kutoa msaada waweze kutoa kwa watu wenye uhitaji Kama vile vyakula na misaada mingine.
katika Dua ya Kuliombea Taifa ilienda sambamba nakushiriki kwa futari iliyoandaliwa na mkuu wa Wilaya hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...