Na Mwandishi wetu, Simanjiro
DIWANI
mstaafu wa Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Clempu
Ole Kinoka ameshinda kesi na kurudishiwa shamba lake la zaidi ya ekari
1,000 lililopo mpakani mwa Kijiji cha Langai na Naberera.
Clempu ameshinda kesi hiyo iliyokuwa kwenye mahakama Kuu ya Mkoa wa Arusha, dhidi ya mfugaji Lenginyu Yamat.Hata hivyo, Mahakama hiyo imeagiza Lenginyu aachalie shamba hilo mara moja na kulipa faini ya shilingi milioni 120.
Klempu ameishukuru Mahakama hiyo kwa kutoa haki yake kwani shamba hilo alipata kihalali kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.Amesema mgogoro kwenye shamba hilo ulianza tangu mwaka 2019 na baadhi ya wanasiasa walichochea ili waichukue ardhi hiyo.
"Namshukuru
Mungu nimefanikiwa kupata tena shamba langu ambalo nilinunua kwa njia
ya halali kwa kufuata sheria tangu awali," amesema Clempu.Mfanyabiashara
wa Naisinyai, Siria Ngodedia amesema anamshukuru Mungu kwani Mahakama
imetenda haki na kurejesha ardhi hiyo kwa Diwani huyo mstaafu.
"Haki
ya mtu haiwezi kwenda bure, Mahakama imeona mahali haki inapaswa
kuwepo, tunamshukuru Mungu kwa hilo kwani mzee amerudishiwa eneo lake na
kazi iendelee," amesema Siria.Mkazi
wa kijiji cha Langai, Ernest Martini amesema siasa chafu ilitaka
kutumika ili kumdhulumu Clempu eneo lake kwani alinunua kihalali shamba
hilo.
"Baadhi ya viongozi
walitumika vibaya na kutaka kudhulumu mali ya Diwani huyo mstaafu wa
kata ya Naisinyai ila Mahakama imetenda haki," amesema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...