Na Said Mwishehe, Michuzi TV
AMETEMA nyongo!Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea kutokana na sauti ya Msemaji wa Klabu ya Simba Haji Manara ambayo imesambaa mtandaoni kama upepo akitoa lawama zake kwa baadhi ya wachambuzi,wajuzi wa mpira na viongozi wa mchezo wa soka.
Katika sauti hiyo ambayo ilianza kusambaa leo mchana wa Mei 10,2021 kwenye magroup ya mitandao ya Kijamii, Manara ameoneka kutema nyongo na kutoa hasira zake baada ya mchezo kati ya Simba ya Yanga kuahirishwa kwasababu ya kikanuni.
Kupitia sauti hiyo Manara anasikika akisema akidai hivi "Katika maisha yangu ya mpira sijawaji kuona kipindi chenye unafiki kama kipindi cha juzi(Mei 8,2021), yaani nimeona unafiki wa kiwango cha mwisho , watu wanaosimamia haki za washabiki , wanaojifanya wachambuzi, wanaojifanya wajuzi wa mpira wote taka taka tupu.
"Yaani mijitu inakaa kutetea timu kukimbia masaa mawili , kwa hoja ya kikanuni, yaani watu nimewadharau , juzi bado kidogo tu bila Magori nilikuwa sitaki tena mambo ya mpira , upuuzi mtupu, yaani watu unaowaamini wanaweza kuelekeza mambo kwenye mpira ni takataka tu, unafiki umewajaa.
"Mnakaa mnatetea ujinga ujinga watu wanakataa kucheza mechi kwa saa mbili , kisa kanuni , washabiki zaidi ya 30,000 , 40,000 wamelipia viingilio, watu wamelipia vifurushi vyao, watu wamelipa ving'amuzi vyao, watu wametoka mbali , hamjali washabiki mnakimbilia kanuni imevunjwa.
"Katiba ya...(akataja timu)imevunjwa , mwaka watatu huu hawafanyi mkutano mkuu mko kimya tu halafu mnajifanya watetezi wa mpira, takataka tupu , ninawaambia ukweli, wala siwaogopi na hakuna wa kunifanya chochote , hakuna anayeniweza.
"Nimeanza kuchambua kabla yenu wote mko matindigwa huko.Mnajifanya mnchambua mpira kumbe wanafiki tu, hamuangalii washabiki , fikiria watu zaidi ya mamilioni wanasubiria mpira, mnabaki mnang'ang'ania kanuni imevunjwa."
Manara kupitia sauti yake hiyo ameendelea kudai kwamba; "Mbona hamtetei Katiba inayovunjwa, mwaka wa tatu huu hawafanyi uchaguzi , mmekalia unafiki lakini la FCC kutwa mko mtandaoni, unafiki , nawaita nyie wanafiki.Watu mamilioni wanasubiria mpira, Serikali imechaga imetoa maelekezo leo mnasema kanuni imevunjwa.
"Leo Katiba haijavujwa kwa kuikiuka TFF , Katiba inasamaje?Lipi kubwa kati ya kanuni na Katiba, mnakaa tu mnafanya unafiki , mnakaa mnakosa barua, mnashindwa kukosoa waliokimbia mechi".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...