KAMPUNI ya simu TECNO imezindua rasmi TECNO Camon 17pro kwa kushirikiana Tigo Tanzania, Coca Cola, DSTV na Atsoko asubuhi ya 5/5/2021. TECNO Camon 17pro sifa yake kuu ikiwa ni MP48 za Camera ya mbele na teknolojia ya 4K video resolution itakuwa ikipatikana sasa katika maduka yote ya simu ikiwa na ofa ya GB78 za internet kutoka Tigo kwa kipindi cha mwaka mzima.

Katika uzinduzi huo Afisa Uhusiano wa TECNO alisema kwamba, “tunayofuraha kwa kujumuika nasi katika uzinduzi huu wa TECNO Camon 17pro tunafahamu ni kwa mda gani mmekuwa mkiisubri kushuhudia majaabu yanayotokana na MP48 za camera ya mbele na MP64 za camera yenye teknolojia ya black na White mode zenye kupatikana kwenye TECNO Camon 17pro.”

Kwa kifupi uzinduzi wa TECNO Camon 17pro ulizinduliwa na washirika wengi ikiwemo Msanii maarufu Elizabeth Michael ambaye alitambulishwa kuwa wa balozi wa simu hii mpya ya TECNO Camon 17pro, “nashukuru TECNO kwa kuniamini kwa mara nyengine tena. Nimekuwa mtumiaji mzuri wa simu za TECNO Camon na nimekuwa nikifuraishwa na ubora wa picha na ukubwa GB 128 + GB 8 za utuzaji kumbukumbu/memory”.

Washirika nao walipata nafasi ya kuongea machache na Mkuu wa kitengo cha bidhaa kutoka Tigo Bwana Mkumbo amewataka watanzania wote kufika katika maduka ya Tigo kuanzia sasa TECNO Camon 17pro inapatika kwa bei rafiki na ofa ya GB 78 kutoka Tigo.

Kwa sasa pindi tu utembeleapo maduka ya TECNO utaburudishwa na kinywaji baridi cha Coca Cola lakini pia utapendezeshwa muonekano wako na Atsoko karibu sana TECNO www.tecnomobile.com na Twende zetu kistaa na Camon 17pro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...