MAKAMU wa Pili wa Raisi wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka washiriki wa kongamano la Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afika (SADC) kujadili kikamilifu mafanikio na  changamoto zinazoikabili jumuiya hiyo .

 Akizungumza katika ufunguzi wa  kongamano la maadhimisho ya miaka arobaini ya SADC huko katika ukumbi wa Kampasi ya Suza Maruhubi Mhe. Hemed amesema ni vyema kuangalia mafanikio ya SADC yalivyosaidia maendeleo ya nchi na jinsi yakujikwamua kutokana na changamoto kwa ustawi wa wananchi.

Alisema kuwa katika kujadili fursa ya Zanzibar ndani ya SADC katika  Kongamano hilo ni vyema washiriki kuchambua na kuonyesha jinsi Zanzibar inavyoweza kutekeleza  na kuimarisha kipaumbele cha Uchumi wa Bluu kupitia Jumuiya hiyo.

Aidha alisema kuna fursa nyingi za kibiashara katika nchi za SADC ambazo zikitumika vizuri zitaisaidia Zanzibar kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa kipindi kifupi.

Alisisisitiza kuwa kongamano hilo  lijikite katika kuchambua kwa kina jinsi  Zanzibar itakavyonufaika kwa lugha yake ya Kiswahili kupitia Jumuiya hiyo na kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa bidhaa inayouzika katika nchi za SADC.

Alisema Zanzibar ikijipanga vizuri itawasaidia Vijana wengi waliohitimu taaluma ya lugha ya Kiswahili kuwapatia fursa za ajira ya kufundisha Kiswahili kama lugha ya pili katika nchi zinazounda Jumuiya hiyo.

Nae Balozi Soud Masoud Balozi amewataka wananchi wa Zanzibar kutumia fursa mbalimbali za kibiashara ambazo zinapatikana katika Jumuiya ya SADC ili kuondokana na umasikini.

Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imeanzishwa 1 april, 1980 huko Lusaka nchini Zambia na ina wanachama ndani ya nchi.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...