Mgeni rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na utawala bora Mhe Mohamed Mchengerwa akipokea  zawadi maalum kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Mwenyekiti wa TAPSEA Zuhura  Songambele  Maganga kwa kuitambua kada hiyo muhimu na yenye mchango mkubwa.Mhe.Mchengerwa amefungua mkutano wa nane wa mwaka wa chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania {TAPSEA} jana katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.Mkutano huo wa Mwaka umewakutanisha Makatibu Mahsusi zaidi ya 3000  kutoka mikoa mbalimbali nchini.Pichani kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongela.
Mwenyekiti wa TAPSEA Zuhura  Songambele  Maganga akimpokea Mgeni rasmi  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na utawala bora Mhe Mohamed Mchengerwa alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo kwa ajili  kufungua mkutano wa chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania {TAPSEA} .Mkutano huo wa Mwaka umewakutanisha Makatibu zaidi ya 2000  kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Baadhi ya Wanachama wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...