Na Shukrani Kawogo, Njombe

Wananchi wilayani Ludewa mkoani Njombe wametakiwa kutumia vyema fursa zilizopo katika maemeo mbalimbalia ya wilaya hiyo pamoja na zilizopo nje ya wilaya ambazo zinaweza kuwaongezea kipato pamoja na kukuza uchumi wa wilaya hiyo.

Hayo ameyasema mtaalam wa masuala ya kiuchumi Lucia Mwaipopo kupitia ofisi ya mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga wakati akitoa elimu ya uchumi kwa vikundi vilivyopo katika kata mbalimbali wilayani humo.

Amesema kuwa watu wa maeneo mengi wamekuwa wakizungukwa na fursa mbalimbali za kiuchumi lakini wao wanaishi katika umasikini kutokana na kutojua jinsi ya kuzitumia fursa hizo na kuwaletea kipato ikiwemo wilaya ya Ludewa ambayo ina fursa nyingi za kilimo pamoja na miradi mikubwa ambayo wananchi wake wanaweza kuitumia na kupelekea kubadili maisha yao.

Aliongeza kuwa endapo wakulima na wafugaji wa wilaya hiyo wataelimishwa jinsi ya kufanya kilimo cha kibiashara ikiwemo kulima mazao ambayo yanaendana na soko lililopo kwa wakati huo vivyo hivyo katika ufugaji pia na itapelekea kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na wilaya kwa ujumla.

“Hii wilaya ina fursa nyingi sana, tukianza na kilimo tunaweza kujikita kwenye kilimo cha mazao ya kimkakati kama kahawa, korosho, parachichi na mengineyo, katika ufugaji tunaweza kujikita katia ufugaji samaki kwenye vizimba ndani ya ziwa nyasa, sambamba na ufugaji wa kuku, ng’ombe pamoja na nguruwe”, Alisema Mwaipopo.

Sanjali na hayo aliongeza kwa kumpongeza mbunge Kamonga  kwa kuwapa nafasi ya kujifunza wananchi wake hivyo amewataka wananchi hao kutumia vyema fursa hiyo ambayo wamependelewa kuipata ambapo kwa sasa imeanza kwa kuvitambua vikundi mbalimbali na mahitaji yake pamoja na fursa zilizopo katika kata hizo na elimu hiyo itaendelea kutolewa kwa awamu kwa kipindi cha miaka miwili.

Akizungumza katika mikutano ya kutoa elimu hiyo iliyofanyika katika baadhi ya kata katibu wa mbunge huyo Alphonce Mwapinga amesema ofisi ya mbunge inatambua umuhimu wa wananchi wake katika kukua kiuchumi hivyo ikaona itoe fursa hiyo kwa wanchi ili waweze kupata elimu kwa kuwaleta mtaalamu wa uchumi ili awape darasa Amesema elimu hiyo inayotolewa itawasaidia wananchi kukuza maendeleo yao binafsi kiuchumi na wilaya kwa ujumla na wanaamini kwa kupitia vikundi hivyo wanavyowapa elimu wanaweza kuwafikia wananchi wengi zaidi.

“ofisi ya mbunge inatambua kwamba vikundi vinafaida kubwa, na ukitaka kumuwezesha mwananchi awe na uchumi mzuri ni lazima apate elimu ya kuendana na mazingara ya hali ya uchumi iliyopo hivyo tunaamini tukitoa elimu kwa kikundi cha watu 30 au zaidi tunaimani itafika nbali kwakuwa watawaelimisha na wenzao”, Alisema Mwapinga.

Aliongeza kwa kuwatangazia neema wananchi wanaoishi katikakata za mwambao mwa ziwa nyasa hasa wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi kuwa mbunge wao Joseph Kamonga anawapambania bungeni ili katika ukanda huo kuweze kuanzishwa vizimba ndani ya ziwa nyasa vya ufugaji wa samaki ili ziwa hilo liweze kutoa samaki wengi zaidi kama maziwa mengine na kukuza uchumi kupitia sekta ya uvuvi.

Amesema programu hiyo itaendeshwa kwa kipindi cha miaka miwili ambapo kila eneo litaelimishwa kulingana na fursa zilizopo huku akitumia mfano wa kilimo cha mihogo kwa ukanda wa mwambao ambao hulima sana kilimo hicho kuwa kutokana na msaada wa mbegu walizopewa na mbunge wao wanapaswa kuzitumia kwa tija kamba ambavo wanavyotumia wenzao wa Butihama ambako mbegu hizo zilitoka.

Ameongeza kuwa wanapaswa kujadili mikakati yao ya kukuza zao hilo kupitia mbegu bora walizopata kwa kuona kwa jinsi gani watafanya biashara kama ni kwa kuuza mihogo yenyewe au kutengeneza bidhaa za chakula zinazptokana na mihogo hiyo.

“Kila jambo linapaswa kufanywa kwa malengo, hutuwezi kutumia mbegu bora kwa kilimo cha mazoea wakati wenzetu wanakuza uchumi wao kupitia mbegu hizo hizo za mihogo, tunapaswa kulima kilimo cha kisasa na chenye tija na maslahi kiuchumi”, Alisema Mwaipopo.

Hata hivyo kwa upande wa madiwani wa kata mbalimbali wamemshukuru mbunge Kamonga kwa proghamu hiyo adhimu sana, huku wananchi wao wakifurahia fursa hiyo na kusema kuwa itawasaidia katika kufanya shughuli zao za kiuchumi kulingana na dunia inavyokwenda.

Maria Swai ni mmoja wa wananchi hao amesema yeye anavikundi viwili ambavyo vinashughulika na kuweka akiba na kukopa hivyo kwa elimu hiyo wanayopata itakuwa na faida kwao kwani wataweza kujitanua zaidi katika shughuli za kiuchumi badala ya kuishia kuweka fedha na kukopa.

Mtaalam wa uchumi Lucia Mwaipopo akiwa amezungukwa na baadhi ya wakikundi wakati alitoa elimu ya uchumi katika kata ya Luhuhu
Baadhi ya wanavikundi kata ya Ludewa wakijiqndikisha baada ya kuwasili kwa ajili ya kupatiwa elimu ya uchumi wangu wilayani Ludewa.

 Katibu wa Mbunge Jimbo la Ludewa Alphonse Mwapinga akiwaeleza wananchi wa kata ya Luilo wilayani Ludewa jinsi Mbunge wao anavyotekeleza ilani ya Chama cha mapinduzi kwa vitendo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...