Raisa Said,Tanga.
Imeelezwa kuwa miradi 67 yenye thamani ya shilingi bilioni 14.323 inatarajiwa kukaguliwa na mingine kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2021 katika Wilaya nane za Mkoa wa Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima ametoa taarifa hiyo leo baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,Salama Mbarouk Khatib.
Amesema ukiwa mkoani Tanga,Mwenge wa Uhuru utakagua miradi hiyo ambayo fedha zake zimetokana na nguvukazi za wananchi,Halmashauri za Wilaya, Miji na Jiji,Serikali kuu na Wahisani wa maendeleo.
Malima amesema mkoa wa Tanga umekuwa wakwanza kukimbiza mwenge wa Uhuru kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara ambapo unatarajiwa kuzindua, kukagua na kuweka majiwe ya msingi katika Miradi mbalimbali yenye thamani ya zaidi shillingi.bilioni 14.323
Aidha Malima amesema kuwa mwenge utakimbizwa kwa siku nane ukianzia katika wilaya yaTanga mjini ,Pangani,Muheza,Mkinga,Lushoto,Handeni,Kilindi,na kumalizikia Korogwe ambapo utakabidhiwa Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu huyo wa Mkoa alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakazi wa jiji la Tanga kujitokeza kwa wingi katika shamrashamra za kukimbiza mwenge wa uhuru huo na katika mkesha utakaofanyika kata ya Mwanzange , mwenge ambao umewasili Mkoani Tanga Lengo kuu likiwa ni kukuza miradi kwa maslahi ya watanzania wote
Akizungumza wakati akikabidhi mwenge wa Uhuru, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Salama Mbarouk amesema mwenge wa uhuru ukiwa huko kwake ulikagua na kuzindua miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.4 katika Wilaya za Wete na Micheweni katika majimbo 9.
Mkuu huyo wa Mkoa Kaskazini Pemba amesema kuwa ameukabidhi Mwenge wa uhuru Mkoani Tanga ukiwa kwenye usalama wa hali ya juu pamoja na jumla ya wakimbiza mwenge kitaifa 6.
Katika makabidhiano hayo kiongozi Luteni Josephine Mwambashi amewataka wakuu wa Mkoa na Wilaya zinazotarajia kupokea Mwenge kuhakikisha wanakabidhiwa nyaraka za miradi wanayokwenda kukagua mapema kabla hawajafika kwenye miradi husika huku akisema hawatakuwa na huruma kwenye miradi itakayodhaniwa kuwa na kasoro.
"Niwasisitize tu kwamba kwenye miradi hasa inayohusu miundombinu na maeneo mengine kutuwahishia mapema nyaraka husika na sio kusubiri mpaka tufike kwenye miradi ndio mtukabidhi, "alisistiza Mwambashi.
Mwenge wa huru unatarajiwa kukimbizwa katika mikoa yote 26 ya Tanzania bara nakwamba ukiwa katika mikoa hiyo itapita katika Wilaya zote za mikoa hiyo.
Hata hivyo ujumbe wa mbio za Mwenge Maalum wa huru kwa mwaka 2021 unaenda sambamba na kauli mbiu "Tehama ni msingi wa Taifa endelevu itumike kwa usahihi na uwajibikaji
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...