Raisa Said,Kilindi

WILAYANI ya Kilindi imeandaa mkakati unaolenga kupunguza idadi ya watu wanaougua ugonjwa wa malaria, hususan miongoni mwa watoto katika Wilaya hiyo Mkoani Tanga.

Akiongea kwenye mahojiano huko Kilindi, Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO), Dk Daniel Chochole alisema kuwa mkakati huo ni pamoja na kutekeleza mpango wa elimu ya uelewa kwa wakazi wa wilaya ili kuondoa imani potofu za jadi ambazo  zinawafanya wakazi wa wilaya hiyo kaacha kutumia vyandarua vilivyowekwa dawa.

Dk Chochole alisema kuwa watu wengine hapa wanaamini kulala kwenye nyavu kunaweza kusababisha kifo au kupunguza uwezo wa wanaume wa kujamiiana.

Wilaya hiyo ilirekodi visa vya ugonjwa wa malaria 75,525 mwaka jana (2020) na karibu nusu yao (32,715) wakiwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO), Dk Daniel Chochole alisema katika mahojiano wagonjwa 48 walifariki na 17 kati yao wakiwa watoto chini ya miaka mitano.

Dk Chochole alisema kuwa idadi ya visa vya malaria vilivyorekodiwa kwa robo ya kwanza ya mwaka huu vilikuwa 16,090 na 4,028 kati yao wakiwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.

“Kulikuwa na vifo 18 katika kipindi hicho na asilimia 50 ya vifo wakiwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano,” alisema na kutoa wito kwa wakazi wa Kilindi kuongeza matumizi ya vyandarua na wananchi wanaposikia dalili  au kuona dalili za malaria wawahi vituo vya afya kwaajili ya matibabu na ushauri zaidi

“Tumesambaza nyavu zilizotolewa bure na serikali. Kuna watu wengine ambao hutumia nyavu kwa ajili ya kulinda mboga kutokanana kushambuliwa na ndege au kutumia kufugia vifaranga vya kuku. Usifanye hivyo, tafadhali. Hizi ni zana muhimu za kuzuia matukio ya malaria katika wilaya, ”alisema.

Dk Chochole aliendelea zaidi kuwa watakutana na waganga wa jadi wilayani humo ili kuwaelimisha juu ya umuhimu wa kuwashauri wateja wao kwenda kwenye vituo vya huduma za afya.

Marimu Shabani ni Mkazi wa Songe mjini Kilindi alieleza kuwa endapo elimu itatolewa katika maeneo yetu utasaidia kupunguza ugonjwa huo hasa kwa watoto wetu .

" Mwaka jana tulimpoteza mtoto wa mdogo wangu sababu ya kuugua malaria hivo elimu hiyo tutakapo ipata itakuwa imekuja  wakati muafaka sababu hawa watoto wetu tunategemea madae waje kuwa msaada kwetu" Alisema Mama huyo 

Dk Daniel Chochole -Mganga Mkuu wilayani Kilindi Mkoani Tanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...