SHIRIKA la Kimataifa la Oxfam limekutana na kutoa mafunzo maalumu ya siku mbili kwa wahariri na waandishi wa habari za kilimo, mafunzo hayo yamelenga kuiinua zaidi sekta ya kilimo kwa kutengeneza daraja baina ya Serikali, wadau mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia, wakulima na wanahabari ambao wana jukumu la kuhakikisha wakulima wanapata taarifa zinazohusiana na sekta ya kilimo pamoja na kuhimiza Serikali kuweka sera rafiki zaidi kwa wakulima.


Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zimejadiliwa na mapendekezo yatokanayo na warsha hiyo yatawafikia wadau lengwa ili kuweza kuimarisha zaidi sekta ya kilimo.

Oxfam international ilianza kufanya kazi nchini Tanzania tangu miaka ya 1960 na wamekuwa wakitekeleza programu mbalimbali ikiwemo uwezeshaji wa wanawake, kukabiliana na umaskini, usawa pamoja na Utawala sawa kwa wote programu hizo zinatekelezwa katika mikoa ya Shinyanga, Morogoro, Loliondo, Arusha na Dar es Salaam.
Afisa wa Ushawishi kutoka Oxfam Tanzania Dkt. George Mwita akitoa mada wakati wa warsha maalumu ya siku mbili iliyowakutanisha Wahariri na waandishi wa habari za kilimo leo Mkoani Dar es Salaam.
Mtaalamu wa miradi ya kidigitali kutoka Oxfam Tanzania, Bill Marwa akitoa mada wakati wa warsha maalumu ya siku mbili iliyowakutanisha Wahariri na waandishi wa habari za kilimo leo Mkoani Dar es Salaam.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari za kilimo wakiwasilisha kazi za makundi wakati wa mafunzo maalumu ya siku mbili yaliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Oxfam.
Baadhi ya wahariri, waandishi wa habari za kilimo pamoja maofisa wa Oxfam Tanzania wakichangia mada wakati wa mafunzo maalumu ya siku mbili yaliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Oxfam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...