Mei
Mosi ni siku ya Wafanyakazi Duniani kote ambapo kitaifa imeongozwa na
Rais wa sita awamu ya 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan zilizofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Matarajio ya wengi ni nyongeza ya mshahara lakini kwangu nimeona Rais
Samia amefanya zaidi ya matarajio kwa Wafanyakazi na hata wasio
Wafanyakazi.
Mosi; Rais
Samia ameshusha kodi ya mshahara ama kodi ya lipa kwa kadri unavyopata
"Pay As You Earn" (PAYEE) kwa asilimia moja (1%) toka 9% hadi kufika 8%.
Hapa maana yake makato ya kodi ya mshahara yamepungua kwa 1% ambapo
kiwango cha mshahara kitaongezeka tofauti na awali ilivyokuwa. Hii ni
sehemu ya nyongeza ya mshahara.
Pili;
Rais Samia amefuta retention fee ya 6% kwenye bodi ya mikopo waliyokuwa
wakikatwa waliokopeshwa fedha za kusoma elimu ya juu. Maana yake kama
ulikopa milioni moja itarudishwa milioni moja na sio milioni moja hiyo
kuongezeka kwa 6% kwa mwaka kama haujamaliza deni lako. Hili ni goli la
ushindi kwa Wafanyakazi wale wenye maumivu ya makato ya fedha za mikopo
kwenye mishahara yao.
Tatu;
Rais Samia amefungua promotion zote ambazo zilikuwa zimekwama tangu
mwaka 2018. Leo hii kuna adjustment ya madaraja kwa wale wenye kustahili
ambao walikosa kufanyiwa hivyo. Maana yake daraja likipanda na mshahara
unapanda pia. Ni neema kwa Watumishi wa muda mrefu kwenye uongezekaji
wa wanachopokea kwenye mishahara yao.
Nne;
Rais Samia ameongeza umri wa utegemezi kutoka miaka 18 hadi miaka 21.
Hii maana yake kuna nyongeza ya manufaa kwa wale wanao wategemea
waajiriwa. Mathalani Mtoto tegemezi aliyekuwa akiishia kupata fursa ya
matibabu ya bima ya afya hadi miaka 18 leo hii atakuwa na nyongeza ya
miaka 3 ya manufaa ya matibabu ya afya. Hapa Rais Samia amemtua mzigo wa
gharama za matibabu kwa Mfanyakazi kwa zaidi ya miaka 3 kwa yule ama
wale wanaomtegemea. Ukitazama utegemezi unaotokana na extended families
zetu utagundua Rais Samia amewaokoa sana Wafanyakazi.
Haya
machache yananifanya nione Rais Samia amefanya zaidi ya matarajio.
Aliyoyafanya Rais Samia ni zaidi ya kupandisha mishahara kwa siku zake
chini ya 50% akiwa Ikulu.
Na Emmanuel J. Shilatu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...