Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge leo May 10 amefuturisha Makundi Mbalimbali ya Wananchi wakiwemo Walemavu wa Viungo, Wasioona, Wasiosikia, Wenye ulemavu wa Ngozi, Wajane, Wasiojiweza, Yatima na Wadau wa maendeleo ambapo Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir Ally ametumia hafla hiyo kutangaza utaratibu wa Sala ya Eid kitaifa na Baraza la Eid.

Mufti wa Tanzania amesema Sala ya Eid kitaifa itasaliwa Viwanja vya Mnazi Mmoja na Baraza la Eid litafanyika Ukumbi wa Karimjee ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa  kuwa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi.

Aidha Mhe. Mufti amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Abubakar Kunenge kwa kuona umuhimu wa kufutarisha Wananchi wa Makundi mbalimbali Jijini humo ambapo amesema kitendo hicho ni sadaka njema mbele za Mungu.

Akizungumza Katika hafla hiyo, RC Kunenge amewashukuru Wananchi walioitika wito wake kwa kujitokeza kwa wingi kuungana nae Katika futari huku akitoa shukrani za dhati pia kwa Wadau walioshirikiana nae kufanikisha Jambo hilo.

Tukio la Iftar ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ilifanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee na kushirikisha mamia ya wananchi wa Dar es salaam.




 






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...