Na.Ashura Mohamed-Arusha
Serikali
Mkoani Arusha imesema kuwa itaendelea kusaidia sekta binafsi ili
ziendelee kufanya vizuri kwa kuwa zimekuwa zikiisaudia Serikali kutoa
ajira.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kiwanja kipya Cha
burudani maarufu kama Tanzanite Lounge kilichopo eneo la fire daraja
mbili Mkoani Arusha,Msaidizi wa mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Enock
Philip Mkumbwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini
Kenani Kihongosi,alisema kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa
kutosha na kuwawezesha wafanyabiashara na wawekezaji katika sekta hiyo
binafsi kufanya shughuli zao katika mazingira wezeshi na rafiki.
"Hawa
ni watu mihimu mno kwa kukuza Uchumi wa wilaya yetu na mkoa wetu na
tunapaswa kuwapa ushirikiano kwa kuhakikisha kuwa Usalama unakuwepo na
mazingira ya kufanya biashara yanakuwa wezeshi kwa kuwa wanatusaidia
sana,kutoa ajira na wanalipa Kodi"alisema Bw.Enock
Alisema serikali wilayani hapo itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na kuhakikisha changamoto ndogo ndogo ambazo zinawakwamisha wafanyabiashara zinakwisha kabisa,kwa Kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Raisi Mh.Samia Suluhu Hassan.
"Niwatake tu Wamiliki wa Tanzanite Lounge muhakikishe kuwa mnatoa huduma bora na za viwango kwa kuwa mpo katika ushindani ili basi kesho na keshokutwa tusikie kuwa mnawekeza katika eneo jingine kwa manufaa ya wananchi wetu na Taifa kwa ujumla"Alisisitiza bw.Mkumbwa.
Aidha
aliwataka Wakazi wa wilaya ya Arusha na mkoa kwa ujumla, kuhakikisha
kuwa wanatembelea eneo hilo kwaajili ya kupata burudani
mbalimbali,Vyakula vya Asili ili kutoa mchango kwa mwekezaji huyo.
Nae
Mkurugenzi wa Tanzanite Lounge bw.Mark Matolo alisema kuwa wamewekeza
katika sekta hiyo ya burudani kwa kuwa jiji la Arusha ni moja ya majiji
yenye sifa zake ikiwa ni pamoja na utalii,hivyo kuwataka Wakazi wa Jiji
la Arusha na viunga vyake kuhakikisha wanafika katika eneo hilo kupata
ladha tofauti tofauti.
Bw.Mark alisema kuwa wamejipanga katika
kuhakikisha kuwa wanaendelea kutoa mchango wao katika sekta hiyo ya
burudani kwa kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora zaidi zenye viwango na
kila mtu atakayefika eneo hilo kuendelea kutamani kufika katika eneo
hilo.
"Tumejipanga vyema na tumeangalia soko linahitaji nini haswa kwa mkoa wetu wa Arusha,kuna vyakula vya asili,kuna vitu vya kuchoma choma Kama kuku na Nyama ya ng'ombe ,mbuzi na burudani hapa patakuwa ndio nyumbani."Alisema Mark
Niwasisitize tu Wakazi wa mkoa wa Arusha na wageni ambao huwa wanatembelea mkoa wetu kuhakikisha kuwa wanafika eneo hili kupata huduma zetu,na tumejipanga vyema kuliko ambavyo wanadhani.
Muonekano wa ndani wa club ya Tanzanite LoungeMsanii wa kizazi kipya Joh Makini mwamba wa kaskazini ambaye nae alihudhuria tukio Hilo la uzinduzi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...