Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wananchi wa mtaa wa Mpeto kata ya Ramadhani mjini Njombe,wameiomba Serikali kuingilia kati kesi ya mtoto wa mtaa huo aliyebakwa akiwa na umri wa miaka 3 mwaka 2018 na kusababishiwa maumivu makali pamoja na kutafutiwa njia mbadala kwa ajili ya haja kubwa na ndogo huku mjomba wake aliyetuhumiwa na kesi hiyo kushinda Mahakamani.

Aidha wameomba serikali kuwachukulia hatua kali wanaume wabakaji na walawiti wa watoto na kuwasababishia ulemavu kufuatia wahusika waliowengi wa matukio hayo ya kikatili kushikiliwa kwa muda na kisha kuachiwa bila kufanywa chochote.

Hayo  yamebainishwa na wananchi hao walipojitekeza katika ofisi ya mtaa huo  kuchangia mtoto wa kike aliyefanyiwa kitendo cha ubakaji  mwaka 2018  na kupata ulemavu ambao unagharimu fedha nyingi kwaajili ya matibabu katika hospitali ya taifa ya Mhimbili.

“Kwasababu wananchi tumekusanyika hapa kwa maana hiyo jambo hili linafahamika kiserikali,kwa hiyo jambo langi la kwanza nitoe rai kwa vyombo vyote vya serikali juu ya hili swala kwasababu sisi tumeonyesha njia kuwa kuna jambo huku na mtoto anahitaji msaada”alisema Alex Mwalongo mkazi wa mtaa huo

Baadhi ya wananchi akiwemo Betrice Malekela mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe na Erasto Ngole Katibu wa siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe,wamesema kuwa vitendo vya ubakaji vinashamiri mkoani Njombe kutokana na jamii kukaa kimya pindi matukio hayo pamoja na kukkubali kuyamaliza katika ngazi ya familia.

“Tumeona kabisa mtoto huyu alivyofanyiwa kwanza ni mtoto mdogo kwa kweli ni kitendo cha ukatili na familia yake ni duni kwa hiyo hapa leo jamii na wanawake wamejitokeza kwa wingi na kupaza sauti ili jamii ijifunze”Alisema Betrece Malekela

Naye Erasto Ngole alisema “Kwa sisi wanaume hiyo ni aibu,mwanaume ameamua kumbaka mtoto mdogo na wanasema wakati huo akiwa na miaka 3”

Wanafamilia akiwemo mama wa mtoto huyo bi,Atu Mkane pamoja na bibi yake wameeleza namna tukio hilo lilivyotokea pamoja na hatua mbalimbali walizochukua.

“Ilifika saa tisa usiku akaja kuniamsha bibi ake akaniambia mtoto umemchukua nikasema hamna tukatoka nje tukaona mtoto amelala nje akiwa amechanika vibaya mno ndio tukaanza kumpeleka zahanati ya Nyombo na kibena ndio matibabu yaikoanzia”alisema mama wa mtoto.

Zaidi ya shilingi milioni 12 za michango ya wananchi zimepatikana kupitia kampeni ya tunaishi nayo inayoendeshwa na moja ya kiuo cha radio wilayani Njombe na kukabidhiwa mama wa mtoto Hakima Kilowoko mkazi wa Mpeto mjini Njombe,kwa ajili ya matibabu yanayoghalimu zaidi ya milioni nne.

Mratibu wa kampeni ya tunaishi nao Ndugu Fikirini Ngailo inayoendeshwa na moja ya radio mjini Njombe akimkabidhi mama wa mtoto aliyefanyiwa ukatili kiasi cha  zaidi ya shilingi milioni 12 ili ziweze kumsaidia katika matibabu ya watoto.
Miongoni mwa fedha zilizokusanywa na wakazi wa mpeto mjini Njombe zikihesabiwa kabla ya kuikabidhi familia kwa ajili ya matibabu ya mtoto.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika hafla ya kuchangi na kukabidhi kiasi cha pesa kwa ajili ya matibabu ya mtoto aliyefanyiwa ukatili mwaka 2018 mjini Njombe. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...