Na. Catherine Sungura, WAMJW-Shinyanga

Mkoa wa Shinyanga umepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 167.4 pamoja na kinga tiba kwa ajili ya zoezi la ugawaji wa kinga tiba hizo kwa halmashauri zote za mkoa huo kwa watoto wenye umri wa kwenda shule.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack wakati wa kufungua kikao kazi cha uraghibishaji na uhamasishaji wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kilichoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele.

Mhe. Telack amesema mkoa wake umejipanga vizuri kwa ajili ya kutekeleza zoezi hilo ambalo linatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu kwa wanafunzi wote wenye umri wa miaka mitano hadi kumi na nne.

Aidha, Mhe. Telack amewataka Wakurugenzi wa halmashauri zote za Shinyanga kuwezesha zoezi la ugawaji wa kinga tiba za Kichocho na Minyoo ya tumbo ili kudhibiti magonjwa hayo na kujenga mazingira mazuri ya kuhakikisha watoto wote wanafikiwa.

“Magonjwa haya yameathiri jamii yetu na kuleta ulemavu hali ambayo imeleta usumbuvu kwa wananchi na watoto kutokuweza kuhudhuria vizuri masomo yao vizuri na kupunguza rasiliamali chache tulizonazo”.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa huyo amewahakikishia wananchi kwamba kinga tiba hizo ni salama na zimethibitishwa na Shrika la Afya Duniani(WHO) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) hivyo kuwataka wale wenye imani potofu kuondoa dhana hiyo.

Vile vile Mhe. Telack amewataka wataalam wa afya na elimu kuwaeleimisha wananchi kwenye maeneo yao kwa kuwapa ujumbe sahihi ili itakapofika zoezi hilo kuweza kutokomeza tatizo hili katika mkoa wao.

Naye Afisa Mradi kutoka Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele, wizara ya afya Bw. Isaac Njau amesema zipo athari nyingi za muda mfupi na mrefu zitokanazo na kichocho kwa wanaume, wanawake na watoto ikiwemo Udumavu, utapiamlo, kuvimba Ini, kuharibika kwa mimba, Kanda ya kibovu Cha miojo pamoja na upungufu wa Damu mwilini.

Bw. Njau alitaja Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele ni pamoja na Usubi,Trackoma,Kichocho,Minyoo ya Tumbo,Matende na Mabusha(Ngirimaji).

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Zainab Telack akifungua kikao kazi Cha uraghibishaji na uhamasishaji wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kwa Viongozi wa Mkoa na Halmashauri zake Kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga.

Baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri wakifuatilia mada Ilizowasilishwa Kwenye kikao kazi hicho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Zainab Telack akiongea na Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt.Yudas Ndungile wakati wa uwasilishaji mada uliofanywa na maofisa kutoka Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele.

Washiriki wa kila kazi hicho wakiwa Kwenye ukumbi huo ambao no Wakuu wa Wilaya,wakurugenzi,waganga wakuu wa wilaya,waratibu wa elimu pamoja na waratibu wa NTD wa Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akifuatilia mada Kwenye kikao hicho.

Afisa Mpango kutoka NTD Bw.Isaac Njau akiwasilisha mada wakati wa uhamasishaji kwa viongozi wa Mkoa na Halmashauri ya Shinyanga ambapo Mkoa huo unatarajia kutoa Kinga tiba za Kichocho na minyoo ya tumbo kwa Watoto wenye umri wa miaka mitano Hadi kumi na nne.


Picha ya pamoja ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na washiriki wa kikao kazi hicho.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...