Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene  akimpongeza Mariamu Salumu kwa kuibuka Mshindi wa Kwanza katika mchezo wa Riadha ya Wanawake ya Mei Mosi iliyomalizika hivi karibuni.Makabidhano hayo yamefanyika leo jijini Dodoma  wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa wizara hiyo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene  akimpongeza Mwanaasha Sungwe kwa kuibuka Mfungaji Bora wa Mpira wa Netiboli katika michezo ya Mei Mosi iliyomalizika hivi karibuni.Makabidhano hayo yamefanyika leo jijini Dodoma  wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa wizara hiyo.

Mkufunzi kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma (TPS), Dkt. Hortensia Kilonzo akiwasilisha mada kuhusu Maisha baada ya Kustaafu kwa wafanyakazi wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi. Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Amani Msuya akizungumza wakati wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu, Abas Malekela akizungumza wakati wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati), akiwaongoza watumishi wa wizara yake kuimba wimbo wa mshikamano wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa wizara hiyo (hawapo pichani).Wapili kulia ni Naibu Waziri, Khamis Hamza Chilo.Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati mstari wa mbele),akiwa kwenye picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa wizara, Watatu Kushoto ni Naibu Waziri Khamis Hamza Chilo na watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara Christopher Kadio. Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...