Pichani Ni Watoto Yatima wa Kito cha UYACHO wakiendelea kufurahia Futari waliyoandaliwa na Tigo.



Sehemu ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano Tigo, katika Picha ya pamoja wakati wa Hafla ya Futari kwa Watoto Yatima wa UYACHO Bukoba.
Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.
Tukiwa tunaelekea ukingoni mwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Kampuni ya Mawasiliano ya Mtandao wa Tigo, Mkoa Kagera wameshiriki Futari ya pamoja na Watoto Yatima wanaolelewa katika Kituo cha Watoto Yatima cha UYACHO.
Kituo hiki kilichopo Kata Hamugembe Manispaa ya Bukoba kimekuwa kikipokea na kulea Watoto tangu Mwaka 1999, kikiendeshwa kwa Hisani za mashirika, Taasisi, watu na misaada mbalimbali, ambapo kwa Sasa Kituo hiki kina jumla ya Watoto 72, huku wengi wao wakiwa wamepitia Kituo hicho, na Sasa wapo katika nafasi nzuri kimaisha.
Akitoa neno la shukrani kwa Niaba ya Bi Saada Kijana wake Sadath Kachwamba, ameipongeza Kampuni ya Tigo kwa kufikiria kushiriki na Watoto Yatima hao, licha ya Fadhila na Thawabu kubwa kiimani wanazopata kutokana na tendo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...