KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua kampeni yake mpya ya ushindani inayokwenda kwa jina la 'Twende Mjini na M-Pesa' ambapo kupitia huduma za M-Pesa zitawawezesha wateja kushinda bodaboda, bajaji na gari jipya aina ya Toyota Corolla Cross (SUV,) huku malengo ya kampeni hiyo yakielezwa ni  kuwashawishi wateja wake kutumia mfumo wa M-pesa ili kumwezesha malipo kwa uhakika.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Mkoani Dar es Salaam Mkurugenzi wa huduma ya M-Pesa Tanzania Epimack Mbeteni amesema, wamekuwa wakiendelea kuongoza katika uboreshaji wa huduma na kwa sasa wateja wa Vodacom kupitia huduma ya M-Pesa 150 00# na M-Pesa App watumiaji wa huduma hizo wanaweza kushiriki na kujipatia nafasi ya kujishindia zawadi hizo kwa kutumia huduma za M-Pesa kwa kutuma pesa kwa wateja wa Vodacom, mitandao mingine au kwenda nje ya nchi na kila muamala utakaofanywa utamwingiza mteja kwenye droo ya ushindani.

"Vilevile ushiriki na kupata nafasi ya kushinda zawadi hizi ni pamoja na kufanya malipo ikiwemo lipa Kampuni, mfanyabiashara au malipo ya mtandaoni na pia kufanya malipo ya Serikali kwa kulipa kodi ya ardhi, LUKU, DAWASCO na TRA.....Kubwa zaidi ni kutumia huduma za kifedha ikiwemo Songesha, M- Pawa na VodaBima." Amesema.

Aidha wateja wa Vodacom kupitia huduma ya M-pesa wanaweza kushinda zawadi hizo kwa kununua vifurushi vya muda wa maongezi kwa kujinunulia wenyewe au rafiki pamoja na kutuma pesa kutoka akaunti ya benki kwenda M-Pesa.

Akifafanua kuhusu zawadi hizo zitakazotolewa ndani ya wiki nane, Mbeteni amesema jumla ya bodaboda 40 pendwa aina ya Boxer BM 125X zitatolewa, Bajaji 8 aina ya TVs King GS na kubwa zaidi katika Grand Finale  gari jipya la 2021nchini na la kisasa aina ya Toyota Corolla Cross (SUV) litatolewa kwa mshindi atakayekuja Mjini kupitia huduma ya M-Pesa.

Mtandao wa Vodacom umekuwa kinara kwa kwa kutoa Mawasiliano na huduma za kifedha mtandaoni, ikiwa na wateja wapatao milioni 15.5 Vodacom imekuwa ikiendeleza juhudi za kufikisha Mawasiliano na utoaji huduma za kifedha kwa njia za mtandao katika maeneo mengi ya nchi.

Mkurugenzi wa Masoko kutoka Vodacom Noel Mazoya, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Twende Mjini na M-Pesa iliyozinduliwa na Kampuni hiyo na kueleza kuwa kwa kutumia huduma za M-Pesa pekee wateja watapata nafasi ya kujishindia zawadi hizo, Leo Mkoani Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa huduma ya M-Pesa ya Vodacom Fredy Angelo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ambayo itadumu kwa wiki nane na ameeleza kuwa zawadi zinazotolewa ni pendwa sokoni na kila mtumiaji wa huduma hizo atajiweka katika nafasi ya ushindi kwa kila huduma ya M-Pesa atakayotumia, Leo Mkoani Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa huduma ya M-Pesa, Tanzania Epimack Mbeteni akizungumza na waandishi wa habari na wadau wengine wa kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mpya ya watumiaji wa huduma ya M-Pesa ya Twende Mjini na M-Pesa ambayo itawezesha watumiaji wa huduma kushinda zawadi kabambe zikiwemo bodaboda na bajaji, leo Mkoani Dar es Salaam.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...