Na Jusline Marco-Arusha

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof.Abel Makubi amewataka waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi ili waweze kuchukuwa tahadhari dhidi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza pamoja na magonjwa ya mlipuko.

Akitoa tsarifa kwa vyombo vya habari Pro.Makubi amesema kuwa ni vyema wananchi wakaendelea kutekeleza mkakati wa  kujikinga na kujilinda na magojwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza ili kuendelea kuimarisha afya na kulinda nchi dhidi ya magonjwa ya mlipuko yanayoibuka.

Aidha wizara inaendelea kuwakumbusha wananchi kuzingatia tahadhari iliyotolewa huvi karibuni ba Mhe.Rais Samia Suluhu ya kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa Covid 19 kutokana na ugonjwa huo kuathiri nchi nyingi ikiwemo nchi ya India ambayo ina muingiliano mkubwa wa kibiashara na nchi mbalimbali.

 "Nchi ya India ni miongoni mwa nchi ni miongoni mwa nchi zinazo athiriwa na uhonjwa huu ambapo taarifa zinaonyesha kuwepo kwa ongezeko kubwa la idadi ya wagonjwa na vifo hivyo watanzania hatuna budi kujipanga na kuendelea kujiandaa kukabiliana na maradhi haya endapo yatayokea."alisema Prof.Makubi

Aliongeza kuwa mpaka sasa imeweza kudhibiti ugonjwa huo kwa kiasi kikubwa na kuepusha adhari kwa wananchi ambapo pia alisema magonjwa ya milipuko kama saratani,sukari na shinikizo la damu yanaendelea kuathiri jamij na kuchangia vifo kwa kiasi kikubwa takribani asilimia 40 hadi 45 kwa sasa ukilinganisha na asilimia 33 kwa miaka 5 iliyopita.

Vilevile alisema serikali kupitia wizara ya afya itaendelea kuwakumbusha wananchi kuchukuwa tahadhari za kujikinga na magonjwa hayo kuanzia ngazi ya familia na mashuleni ikiwemo ufanyaji wa  mazoezi,kupunguza vyakula vya mafuta,chumvi,kuacha kuvuta sigara,kuacha kunywa pombe pamoja na kuacha kuvuta sigara ili kuwakinga watoto na kuwapa mwamko wa kuchikywa hatua hizo wakiwa katika umri mdogo.

Sambamba na hayo alieleza kuwa maambukizi ya UKIMWI yameendelea kupungua hadi kufikia asilimia 4.7 huku idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vikipungua kwa asilomia 48 kuyoka mwaka 2015 ambapo maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu yakipungua kwa asilimia 23 na vifo kqa asilkmia 33 kwa kopindi cha miala 3 iliyopita na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria vikipungua kwa zaidi ya asilimia 60 kati ya mwaka 2015 na mwaka 2020.

 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof.Abel Makubi 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...