Na Woinde Shizza , Michuzi Tv Arusha
Naibu
waziri wa ujenzi na uchukuzi Mwita Waitara ameipongeza bodi ya usajili
makandarasi kwa kuboresha mfuko wa kuwasaidia makandarasi kwa kutoa
thamana milioni 100 kwenda bilioni 50 kama ilivyokuwa awali bila kujali
daraja usajili.
Waitara
alitoa pongezi hizo wakati akifungua mkutano wa mashauriano na wadau wa
sekta ya ujenzi kwa mwaka 2021 ambapo alisema kuwa kutokana na hilo
wizara itaendelea kushirikiana na bodi hiyo ikiwa ni pamoja kuendelea
kuhakikisha miradi isiyozidi bilioni 10 inatekelezwa na makandarasi wa
ndani.
Aliwaeleza kuwa
wanapaswa kuungana na kufunga mkanda wanapopata miradi kwa kuwa
waaminifu na kuhakikisha wanatekeleza kwa wakati pamoja na kuakisi
thamani halisi ya fedha kwani kwa upande wa serikali hawana shida hivyo
waweke mambo yao vizuri.
“Hatuna
shida na usomi wa makandarasi watanzania ila kuna mambo madogodogo
mnapaswa kuyaangali kwani sio malengo ya serikali kukupa kazi alafu
badala ya kufanya kazi hiyo na kutekeleza kwa wakati unaenda kufanya
mambo mengine na mwisho wa siku mradi unakwama,”Alisema Waitara.
Aidha
kuhusiana suala la utekelezaji miradi ya serikali kwa kutumia Force
akaunti ambayo inawanyima fursa makandarasi kupata kazi alisema kuwa
majibu ya suala hilo watalipata rasmi katika mkutano unaofuata
utakaofanyika mwanza kutoka kwa waziri mwenye dhamana Mhandisi Leonard
Chumuriho.
Alifafanua
kuwa Force akaunti ni kwaajili ya kupunguza gharama na kupata matokeo ya
haraka lakini kama wamepunguza gharama na kuendana na hali halisi ya
uchumi wa nchi jambo hilo linazungumzika kwani wanaamini katika utaalamu
lakini tatizo linakuja katika changamoto ya kimahitaji yaliyopo katika
nchi.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa Bodi ya makandarasi Cosolata Ngimbwa alisema
hali ya wakandarasi kiuchumi kwa sasa ni mbaya na yote ni kutokana na
serikali kuamua kutumia Force akaunti ambapo ameiomba serikali kuwapa
nafasi makandarasi kwani wameiva na watajenga katika ubora unahitajika
na kwa wakati.
“Tamisemi
wana kazi nyingi lakini wamewapa local fundi sasa tunaomba wapeni
makandarasi hawa kwani wamejifunza na watafanya kwa bei nzuri na
kumaliza,” Alisema Cosolata.
Sambamba
na hayo aliwataka makandarasi kuacha makundi bali wawe na sauti moja
ambayo itawafanya wakae chini na kuzungumza na serikali na sio kila mtu
kuongea kivyake kwani hawataweza wala kuingia katika miradi hiyo.
Naye
msajili wa bodi hiyo Mhandisi Rhoben Nkori alisema kuwa ka mwaka 2020
wameweza kuwasajili makandarasi 907 na kufanya jumla ya makandarasi
waliosajiliwa kuwa 11749 pamoja na kmiradi 3179 ya ujezi yenye thamani
ya shiliomgi trilioni 3.8 hukub asilimia 96.7 ikiwa imefanywa na
makandarasi wa ndani na asiliia 3.3 ikna maandarasi wa nje.
Alifafanua
kuwa miradi asilimia 96.7 ilikuwa na thmani ya asilimia 46.5
ikilinganishwa na miradi asilimia 3.3 iliyofanywa na wageni kuwa na
thamani ya asilimia 53.3.

Naibu waziri wa
ujenzi na uchukuzi Mwita Waitara akifungua akifungua mkutano wa
mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi kwa mwaka 2021.

Wakandarasi waliohudhuria mkutano huo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...