Na Amiri Kilagalila,Njombe
Shirika
la umeme Tanzania (TANESCO) kupitia idara ya masoko,limeendelea kutoa
elimu ya matumizi bora ya umeme kwa wamiliki wa viwanda na wamiliki wa
mashine za kusaga na kukoboa mkoani Njombe ili waweze kufahamu jinsi ya
kupunguza gharama ambazo si za lazima kwa kununua vifaa vya kisasa na
kuachana na vifaa vilivyochakaa na vya zamani kwani vinatumia umeme
mwingi.
Team ya TANESCO
kutoka makao makuu iliyoambatana na afisa masoko Bi,Jennifer Mgendi na
TANESCO mkoa wa Njombe wamekutana na baadhi ya wamiliki hao na
kuwafikishia elimu kuhusu utaraibu wa kufunga motor za kisasa na
kuzifanyia service mara kwa Mara ili motor iendelee kuwa na ufanisi.
Aidha
wametoa elimu ya usalama wa umeme kwa kuwa nishati hiyo ni nzuri pia
umeme ni hatari kutokana na madhara yanayoweza kutokea baada ya kuwaka
moto unaotokana na sababu mbali mbali.
Vile
vile wataalamu hao wametoa elimu ya kufunga power factor ili iweze
kuwasaidia katika uendeshaji wa mitambo yaani KVA haitakuwa kubwa.
Wamiliki hao pia wameelezwa faida ya matumizi bora ya umeme ukiwa ni pamoja na kuokoa pesa yao.
Ezekiel
Chaula ni mmoja wa wamiliki wa viwanda vidogo anayetumia umeme katika
shughuli zake za uchomeleaji katika kata ya Ilembula wilayani
Wanging'ombe amewashukuru Tanesco kwa elimu hiyo huku akiomba elimu iwe
endelevu
"Kwanza
niwashukuru Tanesco kwa huduma zao wanazozitoa tofauti na kipindi cha
nyuma.Changamoto tunazokutana nazo sasa hivi ni za kawaida na kadri siku
zinavyozidi kwenda zinazidi kuboreshwa"alisema Chaula
Ameongeza
kuwa "Kwasasa hata kama umeme unakatika kwa dharula tunapewa taarifa
mapema sana na kujiandaa tofauti na hapo awali"aliongeza Chaula
Viwanda
vilivyotembelewa mkoani Njombe hususani katika halmashauri ya wilaya ya
Wanging'ombe na Njombe ni pamoja na mashine za kusaga na kukoboa,bakery
na viwanda vidogo vya kukamua alizeti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...