NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA) Shamim Khan, amelishauri Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) liwahusishe wanawake kwenye masuala mbalimbali na kuwapa fursa ya kujielimisha kwenye masuala ya kidunia.

Pia amewataka viongozi wa dini hiyo kuanzia misikitini hadi taifa kuwaunga mkono wanawake na kufanyia kazi kwa vitendo kauli mbiu ya Mufti wa Tanzania, Abubakar Mbwana ‘Jitambue, Badilika Acha Mazoea’ ili kuwawezesha kufikia mabadiliko ya kisayansi na kiteknolojia.

Khan,alitoa kauli hiyo jijini Mwanza jana wakti wa hafla ya kuashua mfumo wa Elimu Masafa (Bakwata Online Academy), akisema wanawake wa Kiislamu ni sehemu ya jamii ya Watanzania, ni vyema wakahusishwa kikamilifu kwenye masuala yote ya Bakwata na kulipongeza baraza hilo kwa kuanzisha na kushua (kuzindua) mfumo wa elimu masafa.

Waziri huyo wa Viwanda na Biashara katika Serikali za Awamu ya Kwanza na ya Pili, alisema wanawake wana matatizo mengi ya kijamii lakini anafarijika kuona elimu masafa kuwafikia akinamama majumbani mwao bila kuathiri majukumu yao.

“Si wengi wanaifahamu elimu hiyo ya kidijitali,kuna pengo kubwa kwa watoto wa kike katika nchi zinazoendelea, hatua madhubuti zinatakiwa zichukuliwe kupunguza pengo hilo,elimu mbalimbali tuipate wote bila kujali jinsia ili wanawake wajifunze na kuingia kwenye uchumi wa kati,kutawaongezea fursa za ajira zenye ajira bora na fursa za kibiashara,”alisema.

Khan alisema wanawake kwa pamoja wanajitahidi licha ya changamoto zinazowakabili,hivyo wasiseme wao ni wanawake bali wathubutu kwa sababu serikali na Bakwata inaruhusu kundi hilo kujielemisha, hivyo akina mama waungwe mkono na viongozi kuanzia ngazi msikiti hadi mkoa ili wajiendeleze na kujielimisha katika masuala ya kidunia.

Alisistiza wanawake na wasichana wasiiache nafasi hiyo kwa sababu dunia ya sasa haitakuwa ya kalamu na karatasi, wasiache fursa hiyo ya masomo ni muhimu kwenda pamoja wanufaike na wasikubali kubaki walalamikaji na watazamaji wanatakiwa wasome na kuwataka wanaume waache wivu na ujinga. 

"Tuwe na wivu wa kimaendeleo,maana elimu si kwa wanaume tu bali na kwa wanawake iwe taaluma yoyote na si lazima uwe rais, unaweza kuwa mhandisi, muuguzi ama daktari,”alisema Khan na kudai katiba ya nchi pia ya katiba ya BAKWATA inawatambua hivyo wapewe fursa na kushirikishwa kwenye masuala mbaiimballi 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania (JUWAKITA) Taifa, Shamim Khan akitumia Katiba ya Bakwata kufikisha ujumbe kwa baraza kutoa furs na kuwashikirisha wanawake kwenye masuala ya baraza hilo jijini Mwanza kabla ya kuinduliwa kwa mfumo wa Elimu Masafa (BAKWATA Online Acdemy).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...