WATOTO ziaid 40 kutoka Klubu za gofu za Mkoa wa Morogoro, Dar es Salaam Gymkhana na mwenyeji Lugalo wanatarajiwa kushiriki Michuano ya watoto (JUNIOR GOLF TOURNAMENT 2021) iliyoandaliwa na klabu ya gofu Lugalo.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika Jumapili Mei 16, 2021 huku ikijihusisha na wachezaji wengine wa riadha kama sehemu ya kuunga mkoni watoto ambao ndio chimbuko la wachezaji wa timu ya Taifa.
Aakizungumzia shindano hilo, Afisa habari wa Krabu ya Gofu Lugalo Kapteni Selemani Semunyu amesema "Kwasasa Klabu inaweka nguvu kubwa katika kuendeleza vipati vya watoto ambavyo kimsingi wamekuwa na uhaba wa mashindano ukilinganisha na makundi mengine."
‘’Hii nafasi nzuri Mei 16,2021 jumapili kutakuwa na mashindano na tunatarajia watoto kutoka klabu ya gofu Morogoro na Klabu ya gofu Dar es Salaam Gykhana na wenyeji hapa Lugalo itakuwa mwanzo wa kuona na kutambua uwezo wao wa nje ya Klabu zao." Amesema Semunyu.
Aidha Mwalimu wa watoo Lugalo, Athuman Chihundu amesema kuwa wao wamejiandaa vizuri kuiwakilisha Klabu na hata kuleta ushindani Mkubwa kwenye gofu.
‘’Unajua mcheza kwao hutunzwa hapa ndio nyumani na hakuna wachezaji watoto wengini Tanzania hii, ni Lugalo tu hawa wengine wanacheza lakini hapa ni chuo." Amesema Chihundu.
Aidha amesema kuwa wanafunzi waliojiandikisha kushiriki katika klabu yake ni 32 na bado wanaendelea kujsajili wengine kwani wao ni wenyeji na wanatakiwa kuonesha mfano kwa uwingi wa wachezaji kuliko vilabu vingine.
‘’Kwa hapa Lugalo washiriki 32 na Juniors wote nilionaosasa hivi ni 45 lakini wale waliofuzu kabisa kuchezaa viwanja tisa wako 16 na wale wanaocheza viwanja vitatu wako saba.’’
Akizungumza leo Mei 14, 2021 katibu wa Chama cha Gofu Tanzania TGU, Boniface Nyiti amesema amefurahishwa na shindano hilo la watoo na hivyo kutoa wito mwa Vilabu vingine kuweka nguvu pia katika kundi hilo kwa uhai wa michezo.
‘’Tumefurahi kuona sasa Klabu inaenda vizuri na sasa kuweka shindano la watoto kwa hiyo sisi kama TGU tumeona tushirikishe na klabu nyingine ili kuleta hamasa.’
Kwa nyakati tofauti moja ya wadhamni wa shindano hilo, Maryanw Mugo na Ken Mbaya wamesema kuwa wataendelea kuweka nguvu katika kundi hilo na kuahidi kutoa fursa kwa wachezaji watoto wanaoshiriki mashindano Kenya na Zimbabwe kwa ufadhili wao.
Mmoja wa wachezaji watoto wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Shufaa Twalib akijiandaa kupiga mpira akiwa kwenye Mazoezi yaliyofanyika Mwisho wa wiki katika viwanja vya klabu ya gofu Lugalo kujiandaa na Mashindano hayo Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...