Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WAZEE wa Mkoa wa Dar es Salaam wametoa mbalimbali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yakiwemo ya kutaka wawemo kwenye vyombo vya maamuzi kama mabaraza ya madiwani na Bunge.

Aidha wazee hao wametoa ombi kwa Rais Samia kwamba pamoja na kuwa na za msamaha kwa ajili ya matibabu bado wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ,hivyo wametoa ombi wawe wanapata matibabu hadi ngazi ya kikanda , rufaa na taifa.

Akizungumza kwa niaba ya wazee hao wa Mkoa wa Dar es Salaam mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan , Mwenyekiti wa Wazee wa mkoa huo Salum Abdallah Matimbwa alianza kwa kueleza wazee wana changamoto mbalimbali,kuhusu tiba kwa wazee wanaishukuru Serikali kwa kutoa kadi za msamaha wa matibabu kwa wazee.

"Hata hivyo wazee wamekuwa wakipata changamoto wanapokwenda hospitali,wazee hawapati baadhi ya vipimo na dawa wakifika hospitali, hivyo tunaomba wazee tupatiwe vipimo vyote stahiki na dawa kwa kadri ya magonjwa yanayowasibu.

"Pili kadi za msamaha kwa matibabu ambazo wazee tumepewa na halmashauri zetu haziruhusu kupata tiba kwenye hospitali za kikanda, rufaa na kitaifa.Hivyo wigo wa huduma upanuliwe kwenye hizo hospitali za kikanda na rufaa na ikiwezekana Muhimbili,"amesema.

Ombi lao la pili, kwa Rais Samia , Matimbwa amesema wanaomba kuwepo na sheria inayohusu wazee."Rais kwa sasa wazee tunayo sera ya wazee iliyotungwa mwaka 2003 ila tangu kipidi hicho hatujawahi kuwa na sheria inayozungumzia muskabali wa wazee kama zilivyo sheria nyingine.

"Sisi wazee tunaomba hii sera ikamilike na itungwe sasa kuwa sheria ili kuwepo haki za wazee ili zilindwe kwa mujibu wa sheria, kama mnavyosema wenyewe uzee dawa lakini pia uzee karahara, tungeni sheria".

Aidha amesema ombi lao la tatu limezungumzia fursa za kiuchumi na kwamba waze wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbali kwenye maisha yao ya kila siku na ili kujikwamua Serikali imekuwa ikitoa mikopo kwa makundi mbalimbali ya wanawake, vijana na watu walemavu,kumekuwepo na asilimia 10 ambayo imetengwa kwa ajili ya makundi hayo.

"Hivyo na sisi wazee tunaomba wazee tuongezwe kwenye makundi hayo tuwe kundi la nne , tunahitaji kupata mikopo kwa ajili ya kujikimu kimaisha".

Matimbwa amezungumzia pia eneo la pensheni kwa wote,ambapo amesema wazee wa Tanzania Bara wanatambua pensheni kwa upande wa Zanzibar."Tunaipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa utaratibu huu, hivyo na sisi wazee wa Tanzania Bara tunaomba ikikupendeza tupate pensheni kama uchumi utaruhusu.

"Ombi la tano kwako Rais, katika usafiri wa umma wazee tunatambua juhudi za Serikali katika kuimarisha sekta ya usafiri, hata hivyo wazee tunapata changamoto mbalimbali, wazee tunaomba kwenye vyombo hivyo vya usafiri wa umma tuwe na viti vya wazee.Aidha vyombo vya umma vihimizwe kubeba wajuu zetu na wanafunzi wote,"amesema.

Mwenyekiti huyo Wazee wa Mkoa wa Dar es Salam, amesema ombi la sita la wazee , kwanza wanampongeza kwa anavyosimamia masuala mbalimbali ya utawala bora katika nchi yetu."Ombi letu wazee tunaomba juhudi hizi ziendelee katika kuendelea kushughulikia matatizo ya watu vikiwemo vyombo vya ulinzi kufuata miongozo waliyojiwekea ili kuondoa malalamiko madogo madogo.

"Ombi la saba linahusu uwakilishi wazee kwenye vyombo vya maamuzi, sisi wazee tunatambua kuna wawakilishi wa makundi mbalimbali kama wanawake,vijana na watu wenye ulemavu lakini sisi wazee hatumo, hivyo wazee tunaomba tuwemo kwenye uwakilishi katika mabaraza hayo kama kwenye baraza la madiwani, bungeni.

"Rais kumekuwepo na wazee ambao wametekelezwa na familia zao kutokana na sababu mbalimbali, hivyo tunaomba Serikali iendelee kuboresha mazingira ya wazee na kuongeza makazi mengine ya wazee,"amesema Matimbwa.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...