WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amempongeza mhitimu wa DIT Shahada ya Umeme Erasto Chiswanu aliyebuni na kutengeneza kiti cha walemavu ambacho hakihitaji kusukumwa.
Ametoa pongezi hizo leo alipotembelea kwenye maonesho ya kilele ya Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2021 yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Aidha, Waziri Mkuu amempongeza pia mbunifu mwingine Adamu Kinyekile aliyebuni mashine ya kumsaidia mkulima kuvuta maji, kupukuchua nafaka, kukoboa na kusaga ambayo inatembea na inamfata mkulima popote alipo.
Mashine hiyo Adamu Kinyekile ametengeneza chini ya usimamizi wa DIT akiwa ni mshindi wa MAKISATU 2019.
Akizungumza wakati akifunga maonesho hayo Waziri Mkuu amesema ameona mmoja wa vijana ametengeneza kiti cha walemavu."Kumbe tunaweza kutengeneza kiti cha umeme badala ya cha kuchanganya kwa mikono na hii imefanywa na kijana wa DIT."
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza jambo baada ya kutembelea na kukagua mitambo mbalimbali iliyobuniwa na kutengenezwa na baadhi ya wahitimu wa DIT
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...