Chama
Cha Mapinduzi kimesema kinaridhishwa na kutambua jitihada kubwa
zinazochukuliwa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta
ya uwekezaji ambapo mazingira ya mazuri ya kuaminika na kuvutia ya
uwekezaji nchini yamepelekea milango ya uchumi wa nchi kuanza
kufunguka kwa kasi jambo ambalo linatoa taswira mpya ya Taifa kupiga
hatua za kimaendeleo.
Katibu wa Halmashauri kuu
ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ameyaeleza hayo makao
makuu ya CCM Dodoma wakati akizungumza na ujumbe wa Watendaji wa ofisi
ya Waziri Mkuu Uwekezaji uliongozwa na Prof Godius Kahyarara.
Amesema
msisitizo na maelekezo ya CCM kwa serikali ni kuhakikisha wanaendelea
kutengeneza fursa za ajira , kukuza uchumi na kuongeza pato la taifa
kupitia uchumi wa viwanda kama ilivyoelekezwa katika ilani ya Uchaguzi
ya CCM 2020-2025.
"Chama Cha Mapinduzi
kinaielekeza Wizara kuendelea kutekeleza mambo yaliyoainishwa katika
Ibara 17, 18, 22 mpaka 32 ambapo kwa mwaka 2020 mumeanza vyema kwa
kuanza kusajili miradi 169 iliyozalisha ajira 10,000 na kufikia April
2021 miradi 150 imesajiliwa ambapo kiwango cha ajira hakijafikia lengo
hapa tuna kazi ya kufanya na maelekezo ya Chama mkajipange vyema"
Alisema Shaka.
Shaka alifahamisha kuwa CCM
inaitaka wizara hiyo kuendelea kuhamasisha sekta binafsi kutumia
sayansi, teknologia na ubunifu ili kuweka mazingira wezeshi kwa
wawekezaji kufanya uwekezaji hasa katika kufanya utafiti wa teknologia
za kisasa 4th industrial revolution.
"Shirikianeni
na wizara ya Fedha kuimarisha huduma za kiuchumi, kifedha na
upatikanaji wa mikopo. Lazima muweke mkazo zaidi katika kuwalinda,
kuwasimamia wawekezaji walioko chini ili waendelee kukua na kuimarika
zaidi na waone nchi yetu ndio sehemu sahihi ya uwekezaji duniani"
Alifahamisha Shaka.
Kwa upande wake Prof.
Kahyarara ameeleza namna wizara hiyo ilivyojipanga kutekeleza maelekezo
ya chama kupitia ilani uchaguzi ya 2020-2025, pamoja na maelekezo ya
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambapo wamepiga hatua kubwa katika kuandaa
mazingira mazuri ya uwekezaji sambamba na kukamilisha maandalizi ya
kuanza kwa kongano za viwanda (industrial parks) ambapo msukumo wa
kipekee umetolewa katika maeneo ya Kibaha, Magu, Manyoni, Kilosa na
Mufindi katika awamu ya kwanza.
"Hali ya uwekezaji nchini sio mbaya tumepiga hatua kubwa muda sio mrefu tutawajuilisha watanzania namna serikali ya Rais Samia ilivyofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo, aidha miradi mikubwa miwili ipo mwishoni kuanza uchakataji wa alizeti na uzalishaji wa sukari ambayo itazalisha ajira 325,000 ambazo zitakuwa ni sehemu ya ukombozi mkubwa kwa vijana" Prof Kahyarara

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...