NA VICTOR MASANGU,CHALINZE

Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Issa amewataka watumishi na wakuu wa idara wote kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuzingatia weledi,nidhamu.kutenda haki bila ya kumwonea mtu yoyote kwa kuzingatia misingi ya Sheria na taratibu.

Kauli hiyo ameitoa wakati alipofanya ziara yake ya kwanza ya kikazi baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na kuamua kuwakutanisha wakuu wote wa idara mbali mbali kutoka halmashauri za Bagamoyo pamoja na Chalinze kwa lengo la kujadili mipango ya kimaendeleo na changamoto zilizopo.

Mkuu huyo ambaye aliongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Bagamoyo amesema kwamba anamshukuru Sana Rais wa awamu ya sita Mama Samia Suluhu kuweza kumuamini kimteuwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo na kuahidi kutoa ushirikiano kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

''Mm lengo langu kubwa na kikao hiki ni kukutana na wakuu wa idara ambao Nina Imani kubwa ndio wataweza kunisaidia katika kutekeleza majukumu yangu ya kila siku lakini kitu kikubwa ni lazima kuwe na nidhamu katika suala zima la uwajibikajk ikiwemo pamoja na kutenda haki kwa kila mmoja,"alisema mkuu huyo.

Pia alibainisha kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha kwamba inawasaidia wananchi kutatua changamoto na kero zao ambazo zinawakabili katika sekta mbali mbali ikiwemo  afya,maji miundonbinu ya barabara,elimu pamoja na Mambo mengine ya msingi.

Aidha mkuu huyo kupitia kikao hicho aliwakumbusha wakuu hao wa idara kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kwamba wanasimamia vizuri ukusanyaji wa mapato na kuziba mianya ya upotevu wa fedha ili kutumiza malengo waliyojiwekea.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa Wilaya aliwataka watumishi hao kuhakikisha kwamba waachana kabisa na tabia ya kukaa maofisini na badala yake wabadilike kwa kuwatembelea wananchi ili kubaini changamoto zinazowakabili.

Pia alisema atahakikisha kwamba anashirikiana bega kwa bega na watumishi wote wa halmashauri za chalinze pamoja na bagamoyo na kuwataka wawe kitu kimoja na kupeana ushauri katika Mambo mbali.mbali.ikiwemo kuwaletea wananchi maendeleo.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni amemuhakikishia mkuu huyo  mpya wa wilaya kumpa sapoti na mshikamano wa Hali ya juu na kwamba nia ya serikali ya awamu ya sita ni kuwaondolea wananchi changamoto zinazowakabili.

Naye mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Posi pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya Bagamoyo Fatma Latu wamempongeza mkuu huyo kwa uamuzi wa kuwakutanisha wakuu wa idara ambao wataweza kuwa kitu kimoja na kuyatekeleza maagizo yote yaliyotolewa.
 
Mkuu wa wilaya mpya ya Bagamoyo wa katikati Zainabu Issa wa katikati akizungumza na wakuu wa idara mbali mbali kutoka Halmashauri za Bagamoyo na Chalinze ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha kwa watumishi ili kujadili Mambo mbali mbali.kulia kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya  Bagamoyo Kasilda Mgeni na kushoto ni mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhani Possi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...