*Atema cheche kwa Watayarishaji wa filamu 

        

     Na.khadija Seif, Michuzi Tv

PROMOTA wa kimataifa nchini Dickson Mkama maarufu kama DMK global awataka waandaaji wa picha jongefu kujitahidi kutengeneza Filamu ambazo Zina viwango ili tuweze kufika soko la kimataifa.


Akizungumza na Michuzi Tv Dmk amesema wakati Mwengine Filamu nyingi zimekua Haina sifa za kuingia kwenye Soko la ushindani kutokana na viwango vya Filamu hiyo kutoweza kukidhi na kuweza kushindanishwa na Filamu zingine za kimataifa.


"Watayarishaji wamekua wakitengeneza Filamu zenye story nzuri za kufundisha jamii lakini kutokana na kiwango cha matayarisho ya Filamu hiyo unakuta sio rafiki na mtu anaeangalia filamu husika."


Hata hivyo Dmk global ametolea ufafanuzi kuhusu Kushindwa kwa Msanii Diamond platinum ambae alikua Miongoni  mwa wasanii walioweza kuwania tuzo za Bet nchini Marekani na kutofanikiwa kushinda huku akiwasihi wasanii na mashabiki kuacha kushikilia bango swala la uzalendo pamoja na kumbeza Msanii huyo .


"Msanii Burna boy ilikua ni asilimia kubwa aweze kushinda tuzo hiyo kutokana na tayari ameweka rekodi ya kushinda tuzo ya Grammy ,hivyo uwezekano wa kushinda za Bet alikua nao lakini kwa upande wa Diamond platinum ametuwakilisha vizuri lazima apongezwe ni hatua kubwa kuona Mtanzania mwemzetu amefika nafasi hiyo na kwa upande wa uzalendo ningependa kuwashauri tu tuache makando linapotokea jambo tuweze Kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha tunatangaza vya kwetu."


Dmk ametolea ufafanuzi kuhusu show ya Davido ambayo ilikua na lengo la kusaidia watoto yatima na Mashuleni.


"Kupitia show ya Davido time Kushirikiana na Kampeni ya Kusaidia watoto wakike kupata taulo za kike na tumeweza kuunga Mkono Kampeni ya "Namthamini nasimama nae" tumeweza kuchangia boksi 20 za taulo za kike kwa upande wa nchi ya Tanzania alikadhalika wenzetu wataweza kusaidia nchi zao huko waliopo."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...