Miongoni mwa zawadi zilizotolewa na Kampuni ya Fimbo cycle katika siku ya watoto (Asas mtoto day out iliyoandaliwa na Mwanadada Dina Marious
 


Na.Khadija Seif, Michuziblog

WANAWAKE Wametakiwa kuiga Mfano mzuri wa Dina Marios katika kuiweka karibu jamii hasa watoto  katika Sekta ya Michezo na Kimasomo.

Akizungumza na Michuzi Tv Meneja Masoko wa Kampuni ya Fimbo cycle Modric Hussein, ambayo Kampuni hiyo ni mojawapo ya wadhamini katika hafla ya watoto (Asas Mtoto day Out) iliyoandaliwa na Mtangazaji wa kipindi Cha uhondo kutoka Efm nchini  amesema wakati Mwengine watoto wanahitaji kujumuika pamoja na kufurahi ili waweze kujifunza vingi kimasomo pamoja na Kimichezo.

"Hafla hii ya "Asas Mtoto day Out" Ina vingi Sana na inawajengea watoto ujasiri kupitia Mashindano mbalimbali yanayofanyika katika siku hiyo hasa Michezo ambapo unakuta watoto wengi hushiriki na kutaka kushinda hivyo kwa namna moja au nyingine inamjengea mtoto uwezo wa kuwa jasiri na mchangamfu."

Hata hivyo Meneja huyo ameeleza msukumo wake wa kutaka Kudhamini hafla hiyo huku akimtaja Dina Marious kuwa mfano wa Mwanamke wa kuigwa katika jamii yetu.

"Ni kwa Mara ya kwanza tumeonelea Kushirikiana na Dada Dina kutoa zawadi kwa watoto wetu hasa walioibuka washindi kupitia Michezo katika jukwaa na tumetoa Baiskeli 5 na tunategemea mwakani kuendelea kutoa udhamini huu na zaidi ya Baiskeli hizi ."

Pia amesema Kampuni hiyo inajushugulisha na bidhaa za usafiri,Chupa za maji pamoja vingine vingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...