Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bwana Nyakimura Muhoji (kulia) akisoma nyaraka mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa umma na wadau kuhusu kero na malalamiko ya kiutumishi, baada ya kuwatembelea Maafisa wa Tume waliokuwa wakipokea changamoto za kiutendaji za watumishi Wilaya ya Kisarawe, Pwani wakati huu wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma pamoja nae ni Maafisa wa Tume Bw. Robert Lwanji (kushoto) na Bibi Florence Kazuva (Picha na PSC).

KATIBU wa Tume ya Utumishi wa Umma Bwana Nyakimura Muhoji (aliyevaa shati katikati) katika picha ya pamoja na Maafisa wa Tume walioshiriki katika kupokea na kusikiliza kero, malalamiko na changamoto za kiutendaji kutoka kwa watumishi wa umma na wadau Wilaya ya Kisarawe-Pwani tarehe 16-18 Juni 2021 katika kuadhimisha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2021. (picha na PSC).



Maafisa wa Tume ya Utumishi wa Umma (kutoka kushoto) Bw. Robert Lwanji, Bw. Lamech Mapunda na Bw. Justine Jackson wakisoma vielelezo mbalimbali vilivyowasilishwa na mdau wa Tume (kulia). Maafisa wa Tume walikuwa Wilaya ya Kisarawe, Pwani kishughulikia kero na malalamiko kutoka kwa watumishi wa umma, katika Kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma, mwaka 2021. (Picha na PSC).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...