SIKU hii ambayo chimbuko lake ni kumbukumbu ya watoto zaidi 2000 waliuawa wakati wakiandamana kupinga ubaguzi wa rangi katika mfumo wa elimu nchini Afrika Kusini mnamo mwaka 1976.
Maadhimisho hayo kwa hapa nchini Tanzania yanafanyika katika ngazi ya Halmashauri ili kuwawezesha wananchi kwa wingi wao kushiriki maadhimisho hayo.*Mkoani Dodoma, Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii inaungana na Mkoa huo kuadhimisha Siku hiyo ambapo pamoja na mambo mengine, Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango atazindua Makao ya Taifa ya Watoto- Kikombo yanayolenga kuwahudumia watoto walio katika mazingira magumu.
Makao hayo yenye uwezo wa kuhudumia watoto 250 kwa wakati mmoja yamejengwa kwa Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Mfuko wa Abbott.
Mwaka huu kaulimbiu ya Siku ya Mtoto wa Afrika inasema, "Tutekeleze ajenda 2040: kwa Afrika inayolinda haki za mtoto."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...