Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV .


AMETEMA nyongo!Hivyo ndivyo unavyoweza kumzungumzia muigizaji maarufu wa filamu nchini Irene Uwoya baada ya kuwaomboa wabongo kupunguza roho mbaya kwani haisaidii kitu chochote.
Haikuishia hapo, Uwoya ameweka wazi kuwa mtu anapokuzidi kubali amekuzidi na wala hakuna sababu ya kutafuta kasoro ambazo hazina kichwa wala miguu.

Uwoya kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema ameeleza hivi "Mtu akikuzidi kubali huyu kanizidi , acha kutafuta kasoro ambazo hazina kichwa wala miguu, wengi wenu mnashindwa kufanikiwa sababu mpo busy kushusha wenzenu na kuwatafutia kasoro badala ya kujiombea mambo yako yaende.

"Baraka zako zipo kwa watu wanavyokuombea sasa wewe toka uzaliwe huna zuri unawazia wenzako vibaya, unatafuta kasoro za watu huwezi kufanikiwa maisha, huo muda unaotumia kuchukia watu embu muombe Mungu abadilishe maisha yako.

"Huwezi kupanda kwa kumshusha mwenzako,utabakia unalalamika tu Mungu nimekukosea wapi , kumbe roho yako mbaya ndio inakuponza , jifunze kwa walio kuzidi acha chuki hazitakusaidia unapoteza baraka zako."


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...