Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea nchini Tanzani Mhe. Kim Yong Sung kulia ni Katibu wa NEC Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Lubinga

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea nchini Tanzania Mhe. Kim Yong Sung.

…………………………………….

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea nchini Tanzani Mhe. Kim Yong Sung.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 9 Juni, 2021 katika Ofisi za CCM Makao Makuu Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, pamoja na mambo mengine Balozi huyo amekutana na Katibu Mkuu kwa lengo la utambulisho na kuendeleza Ushirikiano na Urafiki wa Kihistoria uliopo kati ya Chama Cha Mapinduzi na Chama Tawala cha Wafanyakazi Cha Korea Kaskazini (Workers Party Of Korea).

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga.

Huu ni Muendelezo wa Katibu Mkuu kukutana na Mabalozi wa nchi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania kuendelea kutambulishana na kuendeleza uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na nchi nyingine, ambapo mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu alikutana na Balozi wa China nchini Tanzania.

*ChamaImara*
*KaziIendelee

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera ndugu Katibu Mkuu kwa kukutana na balozi wa Korea kaskazini. Urafiki wetu ni wa kihistoria na sera yetu daima imekuwa kutofungamana na upande wowote. Tusiruhuru Marekani ituchagulie marafiki

    ReplyDelete
  2. 0 Comments? Mbona maoni niliyowasilisha hapa siyaoni hapa? Mmeyatupa kapuni?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...