Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande (wa tatu kushoto) akimsikiliza mtaalamu wa maabara katika kiwanda cha A TO Z cha jijini Arusha alipofanya ziara ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira yam waka 2004.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande akiwa katika ziara ya kukagua kiwanda cha A TO Z cha jijini Arusha alipofanya ziara ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira yam waka 2004.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande (wa tatu kushoto) akikagua karo la kupokea majitaka yanayotoka katika kiwanda cha A TO Z cha jijini Arusha alipofanya ziara ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira yam waka 2004.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande akiwa katika ziara ya kukagua kiwanda cha A TO Z cha jijini Arusha alipofanya ziara ya kukagua uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira yam waka 2004.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande akizungumza na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kaskazini alipowasili jijini humo kwa ziara ya kikazi.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande akizungumza na uongozi kiwanda cha cha A TO Z cha jijini Arusha na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kaskazini alipofanya ziara ya kikazi kiwandani hapo.

(PICHA NA OFISI YA  MAKAMU WA RAIS)

 

Kiwanda cha A TO Z kimeelekezwa kuwa na utaratibu wa kuwasilisha katika Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingra (NEMC) ripoti ya vipimo vya sampuli ya majitaka ili liweze kufanya tathmini kuhusu kiasi cha sumu kinachoweza kuwemo katika maji hayo.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Hassan Chande ametoa maelekezo hayo Juni 12, 2021 alipofanya ziara ya kukagua kiwanda hicho kilichopo jijini Arusha.

Chande alibaini kuwa ripoti inayoandaliwa na wataalamu wa maabara kiwandani hapo huishia kuwasilisha kwa uongozi wa kiwanda pekee bila kuishirikisha Serikali ili wawafanyie tathmini.

“Nimetembelea kiwanda hiki na nimefika kule maabara nimebaini changamoto hasa katika ripoti zenu zinaishia humu ndani, ni sawa na kufanya mtihani halafu ukajisahihishia mwenyewe huwezi kufeli lazima mpeleke ripoti NEMC wawatahmini,” alisema.

Naibu waziri huyo alisema ipo haja ya kiwanda hicho kuwashirikisha wataalamu kutoka Wakala wa Mkemia Mkuu ili kuweza kupata uhakika wa matokeo ya vipimo kama ni sahihi.

Pia aliuelekeza uongozi wa kiwanda hicho kutanua mtambo wa kutibu majitaka akibainisha kuwa ni mdogo ukilinganisha ukubwa wa kiwanda hali inayoweza kusababisha kushindwa kutosheleza mahitaji.

Hata hivyo Chande alipongeza kiwanda cha A TO Z kwa kushiriki katika utunzaji wa mazingira kutokana na ukusanyaji na urejelezaji wa taka unaofanywa kiwandani hapo.

Alisema kuwa hatua ya kukusanya taka mbalimbali husaidia kuweka Jiji la Arusha na nchi kwa ujumla katika hali ya usafi na kutunza mazingira na kuwataka wananchi waendelee kutunza mazingira kwani ndio uhai.

 

 

 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...