NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mbunge
wa Kibaha Mjini Mhe Silyvestry Koka jana amefanya ziara ya kutembelea
shule ya msingi Muungano iliyopo kata ya Kibaha iliyochomwa moto na watu
wasiojulikana hivi karibuni na kuahidi kuchangia madawti 20.
Afisa
mtendaji wa mtaa wa kwamfipa Kuboja Majogoro amemweleza Mbunge kuwa kwa
kushirikiana na wananchi walifanya jitihada kadhaa za kuinusuru ikiwa
ni pamoja na kuwaita jeshi la zimamoto lakn tayari jengo la madarasa
mawili na ofisi yalikuwa yameshaungua.
Koka
baada ya kukagua uharibifu ambao umejitokeza amewahakikishia wananchi
kuwa tayari Halmshauri ya mji kibaha imeshaingiza kiasi Cha shilingi
19,200,000/- kwenye akaunti ya shule kwa ajili ya ukarabati ambao
tumeshaanza.
Pia Koka
alisema kwamba nia ya serikali ni kuhakikisha inabooresha sekta ya elimu
kwa kuwajengea mazingira rafiki wanafunzi ili waweze kufanya vizuri na
kwamba hawezi kulifumbia macho suala la vitendo vya uharifu unaofanyika
hasa kwa kuchoma Moto shule na nyumba za watu.
Wakati
huo huo Mbunge ametembelea wahanga wa ajali ya moto kata ya kongowe
iliyopelekea familia moja kumpoteza kijana wa miaka 22. Akitoa salamu za
rambirambi amewaomba wafiwa kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki
kigumu Cha majonzi.
Kufuatia
matukio hayo ya moto Koka akiwa ziarani humo alimpigia simu OCD Kibaha
kujua kuna mkakati gani wa kuimarisha ulinzi pamoja na kuwaelimisha
wananchi kuwa na ulinzi shirikishi.
Pia
Mbunge Koka amesema amechukizwa na Jambo Hilo la baadhi ya waharifu
kuchoma Moto shule hiyo ya msingi na kuwataja wanachi wa kibaha
kutolifumbia macho hata kidogo na kwamba watoe taarifa na kuwafichua
wale wote ambao wanajihusisha na vitendo hivyo.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wa Kati
Kati akiwa na baadhi ya viongozi wa Chama chama mapinduzi CCM wakati
alipowatembelea wahanga waliounguliwa na nyumba yao kata ya kongowe.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wa kulia
wakati alipokwenda kutembelea shule ya msingi Muungano ambayo ilichomwa
Moto na watu wasiojulikana.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...