MAMA (MWASHABAN) ni miaka kumi na nne (14) bila wewe katika maisha yetu ya kila siku, tunakukumbuka daima. UPENDO uliotuonyesha katika maisha ya kila siku mama hatuna la kusema, umetuacha tukiwa bado tunahitaji mawazo yako. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa muda wote uliokuwa nasi.
Ushauri wako tutaendelea kuufuatilia na mema uliyotufundisha. Daima tutaendelea kukumbuka hekima na busara zako huku tukiwa na tumaini la kuwa siku moja tutaonana nawe pamoja na Maria (IA).
DAIMA huachwi kukumbukwa na Mumeo George Mapango, wanao Mariam(Chuma), Eva (Hawa), Jackson, Rose, Patrick (Said) na Richard, Wadogo zako, Kaka zako, Wakwe zako, Marafiki, Wafanyakazi Wenzako pamoja na Wajukuu zako.
INNA LILLAH WAYNA ILAYH RAJ’IUN
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...