Tume ya Utumishi wa Umma inasikiliza  kero, malalamiko na changamoto zinazowakabili kiutendaji Watumishi wa Umma, Maafisa wa Tume wanahudumia watumishi na wadau katika Shule ya Msingi Chanzige  Wilayani Kisarawe  tarehe 16-18 Juni, 2021 ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2021.

Maafisa wa Tume ya Utumishi wa Umma Bibi Elizabeth Mabula (kushoto) na Bwana Lamech Mapunda (katikati) wakimsikiliza mdau wa Tume aliyefika kupatiwa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi leo Wilayani Kisarawe ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika Wilayani Kisarawe. (Picha na PSC).

Bibi Agness Kapfunsi(kulia) Afisa Utumishi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma akisikiliza changamoto za kiutendaji za kiutumishi kutoka kwa Bwana Elihuruma H. Mohamed (kushoto) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea kufanyika Wilayani Kisarawe.

Bwana Mbegu Kilawe (kushoto) akieleza kero na malalamiko yake ya kiutumishi kwa Maafisa wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bwana Clement Pallangyo (katikati) na Bibi Saada Ibrahim (kulia) leo Wilayani Kisarawe, sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. (Picha na PSC).

Bwana Amas Mahagala (kulia) Afisa Tawala Mwandamizi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma, akisikiliza kero na malalamiko kutoka kwa Bw. Jacob Y. Sengoli (kushoto) kutoka Manerumango Kisarawe, aliyefika Shule ya Msingi Chanzige, Kisarawe kutoa changamoto za kiutendaji kipindi hiki cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, 2021. (Picha na PSC).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...