Na Gift Thadey, Simanjiro
Mkuu
wa Wilaya mstaafu wa Simanjiro, mhandisi Zephania Adrian Chaula na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, RAS Zuwena Omary Jiri wameagwa rasmi
na chama cha wachimbaji wa madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) Tawi la
Mirerani na kukabidhiwa tuzo na Mkuu wa Mkoa huo, Charles Makongoro
Nyerere.
DC mstaafu
mhandisi Chaula na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga (RAS Shinyanga
Zuwena ambaye awali alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya DAS wa Simanjiro,
waliagwa rasmi na MAREMA Tawi la Mirerani kwa kukabidhiwa tuzo na RC
Makongoro kwenye tukio la kuwapa tuzo 19 za aina tatu, wamiliki tisa wa
migodi ya madini ya Tanzanite katika Mji mdogo wa Mirerani.
Hata
hivyo, katika tukio hilo RAS Shinyanga Zuwena alikabidhiwa tuzo hiyo
ila DC mstaafu Simanjiro Chaula hakuwepo na tuzo yake ikakabidhiwa kwa
Kaimu Katibu Tawala wa wilaya hiyo Mussa Waziri.
Akizungumza
baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo RAS Zuwena amewashukuru wadau wote,
wachimbaji madini, viongozi na wananchi wa Simanjiro kwa ujumla kwa
namna walivyofanikisha utendaji kazi wake kipindi akiwa DAS.
Amesema
alipata wepesi wa kutekeleza wajibu wake kutokana na umoja, mshikamano
na upendo uliokuwepo kwa wananchi na viongozi wa Simanjiro hivyo
anawaaga kwa upendo mkubwa na kuwashukuru.
“Nawashukuru
wote ila Katibu wa MAREMA Tawi la Mirerani Rachel Njau na Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya Simanjiro Yefred Myenzi, kwa nafasi ya
kipekee nawashukuru sana kwa namna mlivyokuwa mnanisaidia kutekeleza
maelekezo ya Mkuu wetu wa wilaya,” amesema Zuwena.
Amewaahidi
kuendeleza mazuri yote kwenye nafasi mpya aliyoipata ya RAS Shinyanga
na akamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyomuamini na
kumteua katika kushika nafasi hiyo.
Hata
hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere, amempongeza
RAS Zuwena kwa kuteuliwa na Rais Mama Samia kushika nafasi hiyo hivyo
awakilishe vyema huko Shinyanga kwa heshima ya alipotoka.
“Utakapofanya kazi zako vizuri ukiwa Shinyanga sifa zitakuja Simanjiro na Manyara kwa ujumla ila ukiharibu utasababisha sisi sote tuonekane kuwa tumeharibu nakusihi usije kutuangusha huko Shinyanga,” amesema Makongoro
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, RAS Zuwena Omary Jiri akiwa na mumewe baada ya kukabidhiwa tuzo na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere, kama ishara ya zawadi ya utumishi uliotukuka kwenye nafasi ya Katibu Tawala wa Wilaya DAS Simanjiro iliyotolewa na Chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara, (MAREMA) Tawi la Mirerani.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Charles Makongoro Nyerere, akimkabidhi tuzo Katibu Tawala wa Mkoa RAS Shinyanga, Zuwena Omary Jiri kama ishara ya zawadi ya utumishi uliotukuka kwenye nafasi ya Katibu Tawala wa Wilaya DAS Simanjiro iliyotolewa na Chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara, (MAREMA) Tawi la Mirerani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...