Na Mwandishi wetu, Babati
MBUNGE
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia vyuo vikuu, Dkt
Paulina Nahato amefanya uzinduzi wa safisha kitaa Mjini Babati kwa lengo
la utunzaji wa mazingira yanayozunguka eneo hilo.
Uzinduzi huo umetayarishwa na kampuni ya The Show Case na kushirikisha wananchi mbalimbali wa Mjini Babati.
Dkt
Nahato amewaasa vijana kujali mazingira yanawayozunguka na kujali afya
zao katika kufanya shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo.
"Ukifanya
shughuli zozote za kujiletea maendeleo na ili zifanikiwe unapaswa kuwa
na afya ya kimwili, kiakili, kiroho, na kimahusiano," amesema Dkt
Nahato.
Ameahidi kununua
mapipa madogo ya kuhifadhi taka kwenye baadhi ya maeneo ya mji wa Babati
ili kuunga mkono kampeni hiyo ya safisha kitaa.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa mji wa Babati, Faustine Masunga amesema wanatarajia
kujenga dampo jipya la kisasa ili kufanikisha usafi wa mazingira katika
eneo hilo.
Mratibu wa The
Show Case, Robin Mtasiwa amesema pamoja na kuandaa shughuli hiyo ya
uzinduzi wa safisha kitaa, bila kujali faida, kuna changamoto ya vijana
kutopewa nafasi japokuwa shughuli hiyo ina lenga kunufaisha jamii nzima
na siyo mtu mmoja.
Katibu
wa CCM Wilaya ya Babati Mjini, Fauswali Dauda amewaasa wamachinga kuwa
na utaratibu wa kusafisha mazingira ili wasibughuziwe na viongozi na
kuwapongeza vijana kwa shughuli hiyo na kuwaasa iwe endelevu.
Katibu
wa Jumuiya ya UVCCM Wilaya ya Babati Mjini, Baraka Sultan Mipiko
amesema wiki ijayo wataendeleza usafi wa mazingira kwenye eneo jingine
kwa kusafisha makaburi karibu na Mahakama ya zamani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...