Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MKUU
wa mkoa wa Pwani ,Aboubakar Kunenge ameingilia kati mgogoro wa ardhi
kati ya wakazi wa Mwembengozi kata ya Dutumi pamoja na wizara ya kilimo
,ambapo amehitaji kukaa meza moja na wawakilishi watatu kutoka kwa
wananchi na wataalamu wa ardhi, ili kufanya uhakiki na uthibitisho .
Kufuatia
malalamiko kutoka kwa wananchi hao ,Kunenge amefika kijijini hapo na
kuunda timu itakayokuwa chini ya katibu tawala mkoani hapo.
Alisema ,masuala hayo yanagusa maslahi ya nchi na mtu mmoja mmoja na ustawi wake hivyo yanapaswa kuangaliwa kwa umakini.
"Wananchi
hawa nao wana hoja ,hivyo twende kwenye uhakiki na uthibitisho ,naomba
mungu anisaidie nitende haki " alisisitiza Kunenge.
Kunenge
alielezea kwamba ,timu hiyo itafanya kazi kwa siku moja ,watahakiki
nyaraka ,wataenda kwa hoja kwa kuzingatia sheria ili kupata suluhu na
kufanya maamuzi yenye haki ,:";!Wakati mwingine inahitajika busara na
jambo hili litakwisha.
Awali
,mkazi wa Dutumi Fundi Mbegu ,Ramadhani Kondo,Maua Rashid na bibi Zena
walisema wapo wenye maeneo hapo tangu mwaka 1968 ,vikiwa ni vijiji vya
asili kabla ya ujamaa mwaka 1974.
Walisema
,kijiji hicho cha Mwembengozi kimepimwa ,kipo katika mpango wa matumizi
bora ya ardhi ,na katika nyaraka zote hao kilimo hawaonekani katika
vijiji vyao sasa wanashangaa wanadai haki ni yao na kutaka kuwapora
maeneo yao .
Mbegu alisema ,wakiwa katika eneo hilo ,wizara ilifika kwa wakazi hao kuomba eneo la kupitisha mifugo na sio kujimilikisha.
"Tumelima
mikorosho,mihogo ,miembe,mazao mbalimbali ,Sisi hatuondoki haki
itendeke ,tumekaa hapa miaka mingi ,na sisi ndio tulikutwa na hao kilimo
ikatuomba tuwaonyeshe eneo la kupitisha mifugo ,inakuwaje wanataka
tuondoke tena " walilalamika.
Nae
Maua Rashid alibainisha, walifuata ngazi zote kutoa malalamiko yao
ambapo mgogoro huo ulimalizwa na mkuu wa wilaya miaka hiyo Halima
Kihemba ,na waliishi kwa amani ila amani inataka kuondoshwa baada ya
ofisa tarafa kwenda na Kilimo wakidai ni eneo lao na National housing.
Akitoa
ufafanuzi ,Kamishna wa ardhi msaidizi mkoani Pwani ,Ruth Kabyemera
alieleza,upimaji wa kijiji kitaalamu kijiji kinatangazwa na TAMISEMI .
Ila
kisheria wanamtambua aliyekutwa katika ardhi ,kijiji kikimkuta mtu
katika eneo hakina haki kwani mwenye haki ni aliyekuwapo toka mwanzo
-awali.
Kabyemera alisema
,ufafanuzi huo ni kitaalamu ila hauingiliani na mgogoro uliopo ,hivyo
hatua iliyochukuliwa na mkoa itarajiwe kuleta matokeo chanya ili kila
mmoja awe na amani .
Migogoro
hii ya ardhi ,wakulima na wafugaji huko Kwala ,Dutumi ipo mingi na mkoa
kijumla ,kuna kila sababu ya kuishughulikia ili kuipunguza kama si
kuisha kabisa .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...