* Kamati yampongeza Rais Samia kwa kumteua Basila Mwanukuzi kuwa DC
Khadija Seif, Michuzi TV
MASHINDANO ya kumpata Malkia wa Urembo Wilaya ya Ilala 'Miss Ilala' yamezinduliwa rasmi leo ambapo yanatarajiwa kufanyika Julai 31 mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari mapema leo, muandaaji wa shindano hilo la urembo, Lucas Rutainiwa amesema kuwa mashindano yameanza rasmi kwa kuwa washamaliza usaili wa kuwapata washiriki wa shindano hilo.
"Warembo watakuwa wanakuja mazoezini na kurudi nyumbani hawatakaa kambini hadi siku ya finali na baada ya finali Julai 31 washindi watatu wataenda kuwakilisha ngazi ya Miss Tanzania na tulifanikiwa kupata warembo 17 kwenye usaili."
Washindi hao watakutana na warembo wa Tanzania nzima wakiwemo na wa mikoani na kupatikana mrembo mmoja atakaye iwakilisha Nchi kimataifa katika ngazi ya Dunia Miss World" Amesema Rutainiwa.
Rutainiwa pia amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua muandaaji wa Miss Tanzania, Basila Mwanukuzi kuwa Mkuu wa Wilaya huku akimtaka Basila kufanya kazi kwa bidii na uaminifu ili alinde Imani ya Rais aliyoiweka kwake.
" Kitendo cha Rais Samia kumteua Basila kuwa Mkuu wa Wilaya kinatoa picha ya namna gani tasnia ya Urembo imepiga hatua na inaheshimiwa, ni wajibu wetu tulio katika kiwanda hiki cha Urembo kuilinda Imani hiyo ya Rais wetu," Amesema Rutainiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...