Na Leylah Nassib, DSJ

MTOTO wa msanii maarufu wa Filamu Irene Uwoya Krish Ndikumana amemaliza mafunzo yake ya kwanza ya communion siku ya jana jumapili na kufatiwa na sherehe kubwa ambayo ilifanyika  jioni hiyo na kuhudhuriwa na wasanii wakubwa akiwemo Diamond Platnumz, Aunt Ezekiel, Jackline Wolper, Kajala na mwanaye paula na wengine wengi.

Mama mzazi wa krish, Irene uwoya aliwaeleza waandishi wa habari kuwa;  mafunzo ya communion ya krish aliyafanya kwa kipindi cha miezi sita na kumaliza siku ya jana lakini pia baada ya kuulizwa kwanini hakuonekana akifanya mafunzo hayo alieleza kwamba si kila kitu katika maisha yao ni lazima wakipost katika mitandao ya kijamii hasa mambo ya Mungu na alimaliza kusema anafuraha kubwa na kumshukuru sana Mungu mtoto wake kupata mafunzo hayo.

Licha ya sherehe hiyo pia kulikua pia na maneno mengi pamoja na maoni mengi  kumhusu mtoto huyo kuhusu (mtindo)style yake ya unyoaji kwamba Mama yake hakustahili  kumnyoa style hiyo kwani ni kinyume na maadili yao ya kikanisa na kupitia comments hizo Irene uwoya aliweza kujibu kua Mungu anaangalia moyo na sio kuzungumia style hiyo ya unyoaji kwani ukristo haupo kwenye nywele wala kwenye mavazi ya mtoto wake hivyo hajali watu wakisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...