Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza tarehe 16 hadi 23 Juni 2021, Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa mwaka huu wa 2021 itashiriki zoezi la kugawa vitabu vya kufundishia mtaala wa Uhasibu katika vyuo mbalimbali vinavyofundisha Taaluma ya Uhasibu nchini. Zoezi hilo litahusisha kugawa vitabu kuanzia ngazi zote yaani ngazi ya cheti mpaka Shahada ya juu.

Vitabu hivyo vitakuwa na msaada mkubwa sana kwani vitasaidia waalimu wanaofundisha masomo ya Uhasibu pamoja na wanafunzi wanaosoma fani ya Uhasibu kupata vitabu vya rejea.

Kwa upande wake, Meneja wa Idara ya Elimu na Mafunzo Bw. Peter Lyimo ameeleza umuhimu wa zoezi hilo na kusema kuwa NBAA ina Imani wanafunzi watakaomaliza vyuo na kuja kusoma mitihani ya Uhasibu watafaulu masomo yao kwa kiwango cha juu zaidi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Pius Maneno, ametoa rai kwa waalimu kutumia vitabu hivyo ipasavyo na kuwataka waviweke kwenye Maktaba za vyuo ili wanafunzi waweze kuvipata na kujifunzia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...