Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Jumla ya klabu sita za mchezo wa kuogelea zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya waogeleaji chipukizi (Junior Championships) yaliyopangwa kufanyika kwenye bwawa la kuogelea la Gymkhana Julai 3 na 4.

Klabu hizo ni Dar es Salaam Swimming Club (DSC), Bluefins, Taliss, FK Blue Marlins,   Lake Swim Club na  Mis Piranhas.

Katibu Mkuu wa Chama cha kuogelea Tanzania (TSA)  Inviolata Itatiro amesema kuwa mwisho wa klabu kuthibitisha ushiriki ni kesho na kuziomba klabu ambazo hazijathibitisha kufanya hivyo mara moja.

Alisema kuwa mashindano hayo mpaka sasa yamepata udhamini na Kilombero Sugar Company limited na Tanga Fresh na kutoa wito kwa makampuni mengine kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa Inviolata, mashindano hayo yatashirikisha waogeleaji chipukizi kuanzia miaka 12 kushuka chini na yana lengo la kuibua vipaji vya waogeleaji  kwa ajili ya kushiriki mashindano makubwa na ya kimataifa.

 “Tunawaomba wadhamini wengine wajitokeze ili kufanikisha mashindano haya muhimu kwa maendeleo ya mchezo wa kuogelea nchini. Kuna gharama mbalimbali ikiwa pamoja na uendeshaji wa mashindano pia, siyo kazi rahisi kufanywa na TSA, tunaomba wadau wasaidie,” alisema Inviolata.

Alisema kuwa kila klabu inatakiwa kuorodhesha majina ya waogeleaji wake wakiwa na umri na aina ya mashindano ambayo wanatakiwa kushindana ili kuwawezesha kuandaa programu kamili ya mashindano hayo.

“Mashindano haya yatatoa fursa kwa waogeleaji ambao walishindwa kushindana katika mashindano ya wakubwa kutokana na kigezo cha umri, kwa vile TSA inatambua waogeleaji chipukizi, tumeamua kuandaa mashindano ambao yatawafanya  waogeleaji wanaochipukia nao kujipima uwezo wao,”alisema.

Alisema kuwa kutakuwa na makundi manne, kundi la waogeleaji waliochini ya miaka saba, waogeleaji wa miaka nane na tisa, 10 na 11 na 12. Washindi wa jumla katika kila kundi atazawadiwa kikombe wakati washindi wa kila shindano watapata medali.

waogeleaji chipukizi wakishindana katika mashindano yaliyopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...