Na Karama Kenyunko, Michuzi tv
CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kimeadhimisha wiki ya utumishi Umma kwa wafanyakazi wake (Bonanza Staff ) kwa kufanya mazoezi ya viuongo ili kutunza Afya zao.

Naibu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Dkt. Profesa Prosper Mgaya, ameyasema hayo leo Juni 19, 2021 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya uzunduzi wa bonanza hilo kwa watumishi wote wa chuo lililofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho eneo la Mabibo Mkoani Dar es Salaam. Amesema kuwa wameona kuadhimisha wiki hiyo kwa vitendo kwa kufanya bonanza la michezo.

"Lengo la bonanza hili la Michezo ni kuwaonesha wafanyakazi wetu kuwa ni mhimu kufanya mazoezi ili kuweka afya yako katika hali nzuri."

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Hassani Suluhu amelisisitiza sana hili kwamba ni Vizuri na inapendeza watu wakafanya mazoezi. " Amesema

Amesema kuwa kufanya mazoezi ni vizuri zaidi sio mpaka Daktari akuambie au akuandikie kuwa ufanye mazoezi, lakini wafanyakazi wa Chuo Cha Usafirishaji cha NIT wamelitambua hilo na wameanza kuhamasisha kufanya mazoezi.

Amesema kuwa viongozi wa juu wa Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji wameona wahamasishe wafanyakazi wenzao kufanya mazoezi kwa kila baada ya robo mwaka ili kujiimarisha kimwili, kiakili na kitamaduni wa kufanya mazoezi kila siku.

Hata hivyo ametoa wito kwa jamii kufanya mazoezi kwani ni mazuri kwa kila mtu. "Kwahiyo natoa wito kwa watanzania wote kwamba tufanye mazoezi mazoezi ni dawa ya kuweka mwili wako ukiwa katika afya njema na kwa kufanya mazoezi tunaweza kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza na mangonjwa mengine ambayo hayana msingi wa kukupata.

Kwa upande wa Mkufunzi wa Michezo Chuo Cha NIT Agustino Sakwale amesema kuwa michezo ni burudani michezo ni afya kwani watumishi wote wa NIT wameshiriki bonanza la michezo ili kuendelea kulindaa afya zao.

"Ushiriki wa watumishi wa Chuo cha NITutaimarisha afya zao na pia huongeza ati katika utendaji wa majukumu yao." Amesema Sakwale.

Licha ya hao Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Sara Mwakyusa amesema kuwa amefurahishwa na bonaza kwani watumishi wanatakiwa kufanya mazoezi mara kwa mara kwa ajili ya afya zao.

"Mazoezi haya ni mhimu na mazuri kwani yanawajuisha wote pamoja, tunafurahi pamoja, inatuweka pamoja na tunashirikiana pamoja." Amesema Sara.

Michezo mbalimbali imeshindaniwa katika kuadhimisha bonanza hilo ikiwemo ya Kukimbiza Kuku, kukimbi na yai kwenye kijiko, kukimbia na maguni, mpira wa miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa wavu na mbio za vikwazo na kutunga uzi kwenye sindano huku ukikimbia. Washindi wa michezo hito walijishindia zawadi kemkem zikiwamo pesa taslimu.
Wafanyakazi wa chuo cha Usafarishaji cha Taifa (NIT)wakifanya mazoezi ya kunyoosha viungo ikiwa ni njia moja wapo ya kuadhimisha wiki ya utumishi wa umma katika chuo hicho.
Wafanyakazi wa chuo cha Usafarishaji cha Taifa (NIT) wakikimbia na magunia.
Wafanyakazi wa chuo cha Usafarishaji cha Taifa (NIT) wakivuta kamba.
Wafanyakazi wa chuo cha Usafarishaji cha Taifa (NIT) wakifanya mzoezi mbalimbali ya viungo.
Wafanyakazi wa chuo cha Usafarishaji cha Taifa (NIT) wakiendelea kufanya mazoezi mbalimbali ya viungo.






Wafanyakazi wa chuo cha Usafarishaji cha Taifa (NIT) wakifanya mazoezi ya kunyoosha viungo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...