Bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) inashiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 45 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam ili kuonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Bodi hiyo lililo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango.

Baadhi ya huduma zinazotolewa na PSPTB katika kipindi hiki cha Sabasaba ni kuhuisha taarifa za wanachama wake ( Wataalam wa Ununuzi na Ugavi) kwa njia ya mtandao  online registration system (ORS), kutoa taarifa za madeni ya ada za mwaka za uanachama. Kupitia maonesho ya Sabasaba PSPTB wanatoa elimu kwa wadau jinsi ya kujitengenezea control namba kwa ajili ya kurahisisha ulipaji wa madeni yao.

Akizungumza na Michuzi Blog, Mkuu wa kitengo Cha Masoko na Uhusiano kwa Umma PSPTB Shamim Mdee amesema Bodi hiyo kwa sasa wanatumia mfumo wa kidijitali katika kutoa huduma zake hususan usajili wa wanafunzi na Wanachama kupitia tovuti yao, amesema huduma hizo zinapatikana hata ukiwa sehemu mbalimbali pia kwa sasa huduma hizo wananchi pamoja na wanachama wanaweza kuzipata Sabasaba.
Wafanyakazi wa Bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakiongozwa na Mkuu wa kitengo Cha Masoko na Uhusiano kwa Umma Shamim Mdee wakiwa kwenye picha ya pamoja katika banda la Bodi hiyo katika jengo la Wizara ya Fedha na Mipango.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...