Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia Karatasi yenye majina ya
viongozi mbalimbali walioshiriki kufanikisha kuanza kwa mradi wa Ujenzi
wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka
mkoani Shinyanga km 341 katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza
leo tarehe 14 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha mfano wa kufukia majina ya viongozi mbalimbali walioshiriki kufanikisha kuanza kwa mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe kuweka jiwe la
Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka
Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga katika sherehe zilizofanyika Fela
mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TRC
Masanja Kadogosa kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka
Mwanza hadi Isaka km 341 mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika
sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine wa Chama, Serikali na Bunge, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembea kwenye mfano wa Reli ya
Kisasa itakayojengwa kutoka Mwanza hadi Isaka mara baada ya kuweka jiwe
la msingi katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14
Juni, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa Jiwe la Msingi jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge Railway (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga katika sherehe zilizofanyika Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR ambao utagharimu kiasi cha Shilingi za Kitanzania Trilioni 3.1
Viongozi mbalimbali pamoja na
wananchi wa Mkoa wa Mwanza waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la
Msingi mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR katika eneo la
Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.
Msanii wa Singeli Barobaro akitumbuiza huku viongozi mbalimbali wakimtunza katika Sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi mradi huo mkubwa wa ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR katika eneo la Fela mkoani Mwanza leo tarehe 14 Juni, 2021.
PICHA NA IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...