Na Gift Thadey, Simanjiro
SHULE
ya sekondari ya Mgutwa iliyopo Kata ya Shambarai nje kidogo ya Mji
mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, inatarajia kugawa
na kupanda miche 12,500 ya miti kwenye shule 25 zilizopo Tarafa ya Moipo
ifikapo Mwaka 2025.
Hata
hivyo, Mkurugenzi wa shule ya Sekondari Mgutwa Shedrack Mlemeka amesema
katika kipindi cha mwaka 2016/2017 hadi sasa wamegawa miche ya miti
6,390 kwenye shule 20, ambapo shule 19 zipo Tarafa ya Moipo na shule
moja Kata ya Orkesumet Tarafa ya Naberera.
Mlemeka
ameyasema baada ya mwenge maalum wa uhuru kutembelea na kuzindua mradi
wa hifadhi ya mazingira ya shule ya Sekondari Mgutwa.
Amesema
shule hiyo ni binafsi iliyopo Kata ya Shambarai, Tarafa ya Moipo na ina
walimu 10 na wanafunzi 121, wakiwemo wavulana 61 na wasichana 60
"Tunatarajia eneo hili kuwa la mfano kwa utunzaji wa mazingira kwa jamii zinazotuzunguka na Wilaya kwa ujumla," amesema Mlemeka.
Amesema kwenye shule hiyo ya Mgutwa wamepanda miti 2,000 ambayo imependezesha na kutunza mazingira ya shule hiyo.
Mwalimu wa mazingira wa shule ya Sekondari Mgutwa, Exaud Mafie amesema mradi wa mazingira uliozinduliwa na mwenge umegharimu sh16.7 milioni.
Mafie
amesema katika mradi huo, shule ya Mgutwa imechangia sh8.8 milioni,
Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro sh1.6 milioni, Malihai club sh125,000
na Maivaro Ever Green sh6 milioni.
"Jumuiya
ya shule ya sekondari Mgutwa imefurahi kutembelewa na mwenge wa uhuru
mwaka 2021 na inawatakia safari njema mnapoendelea na shughuli za
kukimbiza mwenge," amesema Mafie.
Amesema
mradi huo unategemea kurejesha uoto wa eneo la shule, upatikanaji wa
kivuli na kuboresha mandhari ya shule kwa ujumla na kupunguza kiwango
cha hewa ya ukaa kilichopo angani na kukabiliana na athari mabadiliko ya
tabia nchi.
Kiongozi wa
mbio za mwenge maalum wa uhuru mwaka huu, Luteni Josephine Paul
Mwambashi akizungumza baada ya kupanda mti kwenye shule ya Sekondari
Mgutwa ameupongeza uongozi wa shule kwa kutunza mazingira.
Luteni
Mwabashi amesema utunzaji huo wa mazingira unapaswa kuigwa na shule
nyingine kwani miti husaidia kuweka mazingira mazuri ya shule.
"Nawapongeza
uongozi wa shule na wanafunzi kwa kutunza mazingira na sisi tumepanda
miti ya kumbukumbu tunatarajia mtaendelea kuitunza kama mlivyofanya,"
amesema Luteni Mwambashi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...