Na.Vero
Ignatus,Arusha
Sera ya elimu bila malipo inamaana kwamba mwanafunzi
atasoma bila mzazi/mlezi kulipa ada wala michango iliyokuwa ikitozwa shuleni
kabla ya kutolewa kwa waraka wa elimu no 5 wa mwaka 2015,ambapo serikali
itagharamia mwanafunzi wa shule ya sekondari na bweni iliyokuwa ikitolewa
na mzazi/mlezi ambapo walikuwa wanalipa ada na michango mbalimbali.
Sera ya
elimu bila malipo ilianza rasmi nchini baada ya serikali ya awamu ya tano
kuingia madarakani mwaka 2015 chini ya hayati Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Sera hii
inamaanisha kufutwa kwa ada zote katika shule za sekondari kuanzia kidato cha
kwanza hadi cha nne na michango ya wazazi katika ngazi ya elimu ya msingi.
Sera hii
imeleta ahueni kubwa kwa wazazi/walezi hasa kulingana na hali duni za kiuchumi
za watanzania walio wengi,Hatua hii imeleta tija kubwa katika sekta ya elimu
nchini kwani inatoa fursa kwa kila mtanzania kupata elimu ya sekondari na
msingi
Pamoja
na sera hii kuleta faida kubwa kwa wazazi lakini imepeleka mzigo mkubwa kwa
wakuu wa shule,Wazazi wengi wanadhani kwamba kwa sasa jukumu la kupata elimu
kwa watoto wao ni la serikali peke yake.
Upande wa
serikali unafanya vyema kutimiza wajibu wake toka sera hii ianzishwe rasmi mwaka
2016. Serikali inatumia fedha nyingi katika utekelezaji wa elimu bila malipo.
Katika
kubaini namna ambavyo sera ya elimu imekuwa ikifanya kazi kwa baadhi ya shule
za msingi na sekondari wilayani Arumeru mkoani Arusha mwandishi wa michuzi blog
aliweza kuzungumza na mkuu wa shule ya sekondari likamba Mwl Juma Tenganija
Bwakwimba ambapo amesema elimu bure inawasaidia wanafunzi kuhudhuria masomo yao
darasani huku akitegemea ufaulu kuwa mkubwa kwa kuwa bado ni shule changa.
Amesema kuwa
elimu bure imekuwa chachu ya kuwafanya wanafunzi kuacha utoro mashuleni kwa
kuwa wana uhakika wa kusoma bure bila ya wazazi au walezi kudaiwa michango yeyote.
Kwa upande
wake mwalimu Richard Mmassy kutoka shule
ya msingi Likamba iliyopo kata ya Musa wilaya ya Arumeru alisema kuwa kutokana
na elimu bure wamekuwa wakifanya vizuri kitaaluma na ufaulu ni mzuri kwa
wanafunzi kwani wanafanya vizuri darasani
Aidha
mwandishi wa blog hii aliweza kuzungumza
na baadhi ya wazazi wenye watoto katika shule hiyo ambapo amenukuliwa akisema:
‘’Kuwa
wamekuwa wakilipia Pesa ya ulinzi na chakula
hii dhana ya Elimu bure sijaelewa kabisa ,kwenye kikao Cha Wazazi tumeitwa
chakula tunalioa 6000 hapo hakuna Elimu bure hayo ,kwa vile wameamua kufanya
hivyo waache wafanye wapendavyo Mimi ninachotaka mtoto wangu asome tu’’.Ni
maneno ya mmoja wawazazi alilalamika
Hata hivyo
kutokana na kauli iliyotolewa hivi karibuni na Naibu Waziri wa ofisi ya Rais
Tamisemi Davide Silinde bungeni Jijini Dodoma inasema kuwa serikali
inatoa elimu bila ada siyo elimu bure hivyo wazazi washiriki kutoa michango
kwaajili ya maendeleo ya shule
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...